img

Watu 9 wafikishwa mahakamani kwa kosa la kuiba korosho gunia 1515 Mkoani Mtwara

January 7, 2021

Na Faruku Ngonyani, Mtwara.

Jeshi la poliis Mkoa wa Mtwara limewafikisha mahakamani watuhumiwa 9 kwa kosa la kula njama ,kuvunja ghala na kuiba korosho gunia 1515  sawa na Kg 105,725 zenye thamani ya sh 163,915,600 ni mali ya kiwanda cha Yalin Cashewnuts company Co ltd kilichopo kata ya mayanga Mtwara Vijini.

Lakini pia tukio lingine jeshi hilo liwashikilia watu 5 wakiwemo viongozi wa chama cha msingi cha mwembetogwa kilichopo Mtwara Vijijini kwa kukutwa na korosho zisizo na ubora gunia 124 sawa na kg 9,920.

Matukio hayo yamethibitishwa na kamanda wa polisi Mkoa wa Mtwara  Mark Njera ACP hii leo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari makao makuu ya jeshi hilo Mkoani Mtwara.

ACP Njera amewataja watuhumiwa waliofikishwa mahakamani kuwa ni pamoja na Yusuph Ally (40) Issa Ismaily Chitanda (24) Ally issa Selemani Limamu (27)Faraji steven Mzuao (36) Hamza Saidi Issa (32).

Wengine ni pamoja Mudy Mohamedi Minjale (27),Hassani Abdallah JumaNdolomi (36) Abilah Issa Mwitau (28) na John Jamal Nyoni (34) dereva na ni Mkazi wa Likone Mkoani Mtewara.

Aidha kamanda wa Polisi ACP Mark Njera ameongeza kuwa kabla ya kubainika kwa tukio hilo la wizi wa korosho walinzi wawili ambao miongoni mwao wapo kweny orodha kutoka kampuni ya Fumwa Security Co LTD waliacha kazi gafla bila kutoa notisi yoyote kwa viongozi wa.

Lakini pia kwa watuhumiwa 5 wanashikilia na jeshi hilo kamanda ACP Njera amewataja kuwa ni pamoja na Ibrahim Mohamed Chisanga (57),Stephano Christopher Stephano(27), Hamisi Hasani Vakuta (24), Salum Hssani Mbaki (49) na Mohamed Ahmad Kandima(28).

Aidha amesema kuwa watuhumiwa hao walikutwa na korosho chafu ghalani wakiwa wamezichanganya na korosho safi ili zionekane zote safi kwa lengo la kuziingiza kwenye msimu wa 2020/21.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amechukua fursa hiyo kwa kutoa wito kwa wananchi wa Mtwara kuacha matendo ya wizi Mkoani humo kwani vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi yake kwa muda ote wa mas

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *