img

Wananchi wa wilaya za mkoa wa Mara kunufaika na bilioni 1.6 za miradi ya maji zilizotolewa na serikali

January 7, 2021

 

Na Timothy Itembe MARA.

WANANCHI ndani ya wilaya ambazo zinaunda mkoani Mara mbioni kunufaika na shilingi bilioni,1.6 ziliizotolewa na Wizara ya Maji RUWASA ili kutekeleza miradi.

Akiongea,Waziri wa Maji,Juma Aweso mbele ya wananchi waliohudhuria katika ziara yake ya kukagua miradi mkoani Mara alisema kuwa serikali imejipanga kutekeleza sera ya maji kumtua mama ndoa kichwani ambapo kila wilaya ndani ya mkoa Mara imetengewa shilingi bilioni,1.6.

Aweso alisema hayo baada ya kusomewa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maji kusuasua katika mkoa Mara ambapo aliwataka wahandisi ambao niwazembe kuachia ngazi kabla rungu la utumbuaji halijawafikia.

Waziri huyo alitumia nafasi hiyo kuwaahidi Wananchi wa wilaya Rorya kuwaletea gari kwa ajili ya kushugulikia uhapa wa changamoto zinazokumba huduma ya upatikanaji wa maji  na siovinginevyo.

“Wizara ya Maji imetoa gari ili kusaidia huduma za maji Wilaya ya Rorya mkoa wa Mara  ambapo watalipata ndani siku tatu kuanzia leo hiyo nikutokana na changamoto  kubwa niliyosomewa ambayo inasababisha miradi ya maji kuchelewa  kukamilika kwa wakati kutokana na umbali mrefu kushindwa uliopo kuifikia”alisema Aweso.

“Hatuwezi kushindwa kutekeleza huduma za Wananchi kwa sababu ya ukosefu wa gari  wizara italeta gari kwa ajili ya kusaidia ufuatiliaji wa miradi hii na hata hivyo Kuna gari zinakuja lazima moja liletwe huku”alisema waziri Aweso.

Waziri huyo alitumia nafasi hiyo kutembelea miradi ya maji iliyopo ndani ya  vijiji vya  Komuge,Kiamwami,kirogo na shirati wilayani hapo.

Kwa upande wake Mhandisi Evaristo Mgaya  akitoa taarifa ya mradi wa maji wa Komuge, alisema mradi huo ulianza toka mwaka 1975 kwa ajili ya Vijiji vya Kyamwame,Komuge,kuruya,irienyi na Baraki ambapo ulikwama kutoa huduma ya maji  mwaka 2009 kutokana na uchakavu wa bomba kuu la kusambazia Maji.

Mgaya alizitaja mojawapo ya changamoto zinazowakwamisha kuwa ni pamoja  na uhaba wa magari kwa ajili ya usafiri wa uhakika kwa ufuatiliaji na usimamizi, Mazingira ya kufanyiwa kazi kutofika kirahisi na kuchelewa kurudishwa kwa huduma ya umeme.

Naye Mbunge wa jimbo la Rorya  Jafari Chege alimuomba Waziri wa Maji kuwarudisha wakandarasi waliokuwa na tenda hapo awali na tayari walikwisha lipwa fedha zaidi ya asilimia 80 ya fedha  anazodai waweze kumalizia miradi sehemu iliyobaki badala ya kumleta mkandarasi mpya ambaye atalazimika kugharimu pesa nyingine.

Chege alisema kuwa changamoto inakwamisha miradi kumalizika kwa wakati ni kutokana na ucheweshwaji wa vifaa  hususani mabomba ya usambazaji wa maji.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *