img

Viongozi wa ulimwengu washutumu hatua ya wafuasi wa Trump kuvamia bunge la Marekani

January 7, 2021

Viongozi mbalimbali ulimwenguni wameshutumu uvamizi wa majengo ya bunge nchini Marekani uliofanywa na wafuasi wa Rais Donald Trump.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa matukio hayo yanafedhehesha, na kwamba Marekani inasimamia demokrasia ulimwenguni kote kwa hivyo ni muhimu kuwa na makabidhiano ya amani ya madaraka.

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema amesikitishwa na matukio katika majengo ya bunge ya Marekani yaliyoko Capitol Hill. 

Kupitia msemaji wake Stephanie Dujarric, Guterres ameongeza kuwa katika hali kama hiyo ni muhimu kwa viongozi wa kisiasa kuwahimiza wafuasi wao kujiepusha na vurugu na kuheshimu michakato ya kidemokrasia pamoja na sheria.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Heiko Maas naye ameandika kwenye ukurasa wa Twitter kwamba kutoheshimu taasisi za kidemokrasia husababisha madhara mabaya.

Marais wa zamani wa Marekani Barrack Obama, George Bush na Bill Clinton pia wameshutumu uvamizi huo wa jana wakisema ni aibu na siasa hatari dhidi ya demokrasia.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *