img

Uchaguzi wa Marekani 2020: Viongozi duniani wazungumza kuhusu maandamano nchini humo

January 7, 2021

Dakika 3 zilizopita

Boris Johnson
Maelezo ya picha,

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson

Viongozi wengi wametoa wito wa amani na ubadilishanaji wa madaraka kwa njia ya utulivu, wakielezea uvamizi uliotokea kama wenye “kuogofya na uvamizi wa demokrasia”.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, amelaani kitendo hicho na kusema ni “aibu”.

“Marekani inasimamia demokrasia kote duniani na ni muhimu sana kuwa na ubadilishanaji wa madaraka kwa njia ya amani na wenye mpangilio,” ameandika kwenye mtandao wa Twitter.

Viongozi wengine wa kisiasa Marekani wamekosoa ghasia hizo huku kiongozi wa upinzani Sir Keir Starmer akitaja kitendo hicho kama “uvamizi wa moja kwa moja wa demokrasia”.

Wazriri wa kwanza wa Scotland Nicola Sturgeon ameandika kuwa kinachotokea bungeni “kinatia hofu mno”.

wafuasi wa rais wa Marekani Donald trump walivamia jumba la Capitol

Maelezo ya picha,

wafuasi wa rais wa Marekani Donald trump walivamia jumba la Capitol

Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sánchez amesema: “Nina imani na demokrasia ya Marekani. Uongozi wa rais mpya Joe Biden utakabiliana na kipindi hiki kigumu, kuunganisha watu wa Marekani.”

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amelaani kitendo hicho na kusema ni “uvamizi mbaya dhidi ya demokrasia”, huku mwenzake wa Ujerumani, Heiko Maas, akisema bwana Trump na wafuasi wake “lazima wakubali uamuzi wa wapiga kura wa Marekani na waache kutatiza demokrasia”.

Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel amesema kuwa aliamini sana Marekani “katika kuhakikisha ubadilishanaji wa madaraka kwa njia ya amani” kwa Bwana Biden, na Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen amesema ana matarajio makubwa ya ushirikiano na chama cha Democrat.

Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg aliungana na wale waliosema matokeo ya uchaguzi ni lazima yaheshimiwe.

Waandamanaji waliingia na kutawala jengo la bunge

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema raia wake “wamehuzunishwa sana na kitendo hicho cha uvamizi wa demokrasia”.

Kipande cha Mwisho cha world leaders.

“Ghasia haiwezi kufaulu katika kupiku mapenzi ya watu. Demokrasia Marekani lazima iendelezwe – na itakuwa hivyo,” ameandika kwenye mtandao w Twitter.

Kutoka New Zealand, Waziri Mkuu Jacinda Ardern, ameandika “demokrasia – haki ya watu kupiga kura, kusikika kwa wanachosema na kufanya maamuzi yao kwa njia ya amani – kusiondolewe kwa kutenda uhalifu”.

Nchini India,Narendra Modi amesema “amesikitika baada ya kuona taarifa za ghasia na vurugu” mjini Washington na kutoa wito kuwa”ubadilishanaji wa madaraka kwa njia ya amani lazima uendelee”

Waziri wa Uturuki wa mambo ya nje ameomba pande zote kujizuia kusababisha vurugu.

Hadi kufikia sasa nchi mbalimbali duniani zimetoa tamko kuhusiana na ghasia hizo ikiwemo Venezuela, Chile, Japani, na Singapore.

Kutoka Fiji, Waziri Mkuu Frank Bainimarama, aliyeongoza mapinduzi yaliyotokea mwaka 2006, pia naye ameonesha kukasirishwa na kilichotokea Marekani.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *