img

Uchaguzi wa Marekani 2020: Mtu mmoja afariki baada ya wafuasi wa Trump kuvamia bunge

January 7, 2021

Dakika 3 zilizopita

wafuasi wa rais donald Trump wakiwa capitol hil

Polisi imethibitisha kuwa mwanamke mmoja aliyepigwa risasi wakati wa vurugu zilizotokea baada ya wafuasi wa Trump kuvamia bunge, amefariki dunia kwasababu ya majeraha aliyopata.

Bado maafisa hawajataja jina la mwanamke huyo lakini polisi wanasema alikuwa raia wa kawaida.

Aidha, mtu mwingine amepigwa risasi wakati wa vurugu zilizotokea ndani ya bunge la Marekani, kulingana na shirika la habari la Associated Press.

Lindsay Watts, mwanahabari wa shirika lenye kuhusishwa na Fox News, ameandika ujumbe kwenye Twitter kuwa wahudumu wa afya wa DC walisema juhudi za kumuokoa mwanamke mmoja aliye kwenye hali mahututi zinaendelea baada ya kupigwa risasi kifuani.

Inasemekana hadi kufikia sasa watu 13 na silaha tano zimenaswa na polisi wakati ghasia zinaendelea bungeni.

Maafisa polisi wa Washington DC wamesema wamepata bunduki tano ikiwemo za mkononi na ndefu.

Mkuu wa polisi Robert Contee amewaambia wanahabari kuwa waliokamatwa sio wakazi wa eneo la DC.

Pia amethbitisha kuwa baadhi ya maafisa wanapata matibabu baada ya kujeruhiwa.

Wafuasi wa Donald Trump wenye hasira wamevuka mipaka ya usalama iliyowekwa na kusimama kandokando ya bunge huko Washington, wakati wabunge wanakutana kumuidhinisha rais mteule Joe Biden kama mshindi wa uchaguzi uliofanyika Novemba mwaka jana.

Katika matukio ya kutatanisha, waandamanaji walizunguka jengo la bunge huku wabunge nao wakisindikizwa kutoka bungeni humo na polisi.

Bwana Biden alisema huo ni “uasi”, huku Bwana Trump kwa upande wake akatoa ujumbe kwa njia ya video akiwataka wafuasi wake kutoka bungeni na kurejea nyumbani.

Kikao cha pamoja cha bunge kuidhinisha ushindi wa Bwana Biden kimeahirishwa na bunge limelazika kwenda mapumzikoni.

Kuna taarifa kuwa watu walitumia bunduki kwenye jengo hilo na mtu mmoja ameuawa.

Mwanamke mmoja anasemekana kuwa katika hali mahututi huku polisi kadhaa wakijeruhiwa.

Aidha, makabiliano yenye kuhusisha silaha yameshuhudiwa katika milango ya kuingia bunge la Wawakilishi.

Pia mabomu ya kutoa machozi yametumika kutawanya waandamanaji.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *