img

Nyota wa Yanga wagomea hoteli maalum waliyoandaliwa zanzibar

January 7, 2021

 

IMEELEZWA kuwa baadhi ya mastaa wa Yanga wamegomea hoteli maalum waliyoandaliwa na waandaaji wa michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Hiyoni baada ya kikosi cha timu hiyo kitue Unguja, Zanzibar kwa ajili ya Michuano ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Jumhuri FC.

Mchezo huo ulikamilika kwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Amaan, visiwani humo saa 2:15 usiku.

Mastaa wa Yanga ni Saidi Ntibazonkiza ‘Saidoo’, Carlos Fernandez ‘Carlinhos’, Tuisila Kisinda, Mukoko Tonombe, Michael Sarpong na Yacouba ‘Songne’.

Taarifa kutoka ndani ya Benchi la Ufundi la Yanga, viongozi nao waliungana na wachezaji hao.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa sababu ya kukataa hoteli hiyo ni kutokuwa na hadhi ambapo haijatumika tangu janga la Corona lilipovamia hapa nchini, hivyo mazingira siyo rafiki kwa matumizi ya binadamu.

Aliongeza kuwa mara baada ya kugoma, haraka waandaaji wa michuano hiyo wakawabadilishia hoteli Yanga.

“Waandaaji walishindwa kuitofautisha Yanga na klabu nyingine shiriki, awali waliwaandalia moja ya hoteli ambayo ni ndogo, haina hadhi ya kutumiwa na wachezaji wake mastaa kutoka nje ya nchi.

“Kwani mara baada ya kutua Zanzibar walipelekwa kwenye moja ya hoteli iliyoandaliwa na waandaaji wa michuano hiyo, lakini walipofika viongozi na wachezaji waliigomea na kuomba wabadilishiwe.

“Walivyogomea haraka waandaaji wakawapa hoteli nyingine yenye hadhi watakayoitumia kwa kipindi chote ambacho Yanga itakuwepo huko ikishiriki michuano hiyo,” alisema mtoa taarifa huyo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *