img

Msafara wa mgombea urais Uganda washambuliwa kwa risasi

January 7, 2021

Polisi mmoja nchini Uganda anazuiliwa katika kituo cha polisi kwasababu ya kuupiga risasi msafara wa mgombea wa urais, Patrick Amuriat, Jumatano magharibi mwa eneo la Kitagwenda.

Polisi imesema afisa aliyekamatwa hakuwa amepewa jukumu la kumfuata Bwana Amuriat katika msafara wake wa kampeni, kulingana na taarifa ya gazeti la Daily Monitor.

Kituo cha televisheni cha eneo NTV, kimeandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter unaoonesha kilichofuata baada ya tukio hilo.

Raia wa Uganda Alhamisi ijayo watapiga kura kuchagua wabunge na rais huku Rais Yoweri Museveni akitafuta kuchaguliwa tena kwa muhula wa sita.

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameshutumu vikosi vya usalama kwa kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa maandamano na mikutano ya kisiasa.

Mwezi uliopia, mlinzi wa mgombea mwingine wa kisiasa Bobi Wine, alifariki dunia baada ya kukanyagwa na gari la jeshi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *