img

Mjini Magharibi yaingia Fainali baada ya kuifunga Mbeya

January 7, 2021

Na John Walter-Manyara

Mashindano ya Taifa (TAIFACUP2021) yanaelekea ukingoni ambapo timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya Nusu fainali ni Mjini Magharibi na Mbeya.

Katika kipute kilichopigwa jioni timu kutoka Mjini Magharibi iliibuka na Mabao 40-37 dhidi ya Mbeya.

Naibu katibu mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) Hilda Mwakatobe amesema kwa ushindi huo Mjini Magharibi itakutana na Arusha kwenye fainali alhamisi ya leo katika uwanja wa Kwaraa mjini Babati.

Mikoa 11 imeshiriki mashindano hayo ya ligi kuu ya Netiboli  yanayoratibiwa na CHANETA huku mwenyeji akiwa mkoa wa Manyara.

Nahodha msaidizi wa timu ya Mjini Magharibi Justina John amesema matumaini yao ni kuchukua ushindi kwa kuwa wamekuja kushindana na sio kushiriki.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufika tamati Leo alhamisi January 7,2021.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *