img

Jinsi ndugu sita na simba wao walivyowatesa wakazi Libya

January 7, 2021

Dakika 6 zilizopita

Two of the brothers' lions
1px transparent line

Kwa miaka kadhaa walifahamika kama familia kutoka jehanamu. Hadi msimu wa joto uliyopita, Mandugu wa Kani waliudhibiti mji mdogo Libya, kuwaua wanaume , wanawake na watoto kudumisha mamlaka yao. Sa uhalifu wao umeanza kufichuliwa pole pole.

Kwa miaka saba wafanyakazi, waliovalia suti nyeupe za kujilinda dhidi ya kemikali wamekuwa wakirejea katika mji mdogo wa kilimo Tarhuna, uliopo kusini- mashariki mwa mji kuu wa Libya, Tripoli.

Wameweka alama katika ploti ambazo wametoa miili 120 kwa kutumia tepu nyekundu na nyeupe japo sehemu kubwa ya ardhi hiyo haijaguswa.

“Kila wakati ninapochimba mwili mpya, najaribu kufanya hivyo kwa umakini kadri ya uwezo wangu,” anasema mmoja wa wafanyakazi wa, Wadah al-Keesh. “Tunaamini kwamba tukivunja mfupa, roho yake itasikia.”

Baadi ya miili hiyo inasadikiwa kuwa ya wapiganaji wadogo waliouawa vitani karibu na Tarhuna msimu uliyopita wa joto, katika mwaka wa tisa wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Libya.

Lakini wengi wao ni raia – wakiwemo wanawake na watoto wadogo waliyo na umri wa hadi maka mitano – baadhi yao wakiwa na alama za kuteswa.

Makaburi hayo ni ishara inayoangazia utawala wa ugaidi uliyodumu kwa karibu miaka minane, ukiendeshwa na familia ya Kanis, na wanamgambo wao.

Watatu kati ya ndugu saba wa Kani wamefariki, na wengine walitoroka mwezi Juni mwaka 2020 bade ya kushambuliwa na vikosi tiifu kwa Serikali ya Muungano ya Libya(GNU) inayotambuliwa na Umoja wa mataifa, lakini mpaka sasa wakazi wa Tarhuna wanaogopa kuzungumzia uhalifu wao.

Baadhi yao wanasema kuwa wanatishiwa na wafuasi wa ndugu wa Kani.

Kukusanya pamoja taarifa kuwahusu ndugu hao – Abdul-Khaliq, Mohammed, Muammar, Abdul-Rahim, Mohsen, Ali na Abdul-Adhim sio mambo rahisi.

Lakini kutokana na simulizi za kuogofya kutoka kwa watu waliowajua, familia hiyo masikini ilitumia ghasia iliyokumba Libya baada ya mapinduzi ya mwaka 2011dhidi ya, Kanali Muammar Gaddafi – na kuongoza jamii yao kwa kutumia ukatili mkubwa.

“Ndugu hao sabawalikuwa wabaya sana na wala hawakuwa na ustaarabu katika jamii,” anasema Hamza Dila’ab, wakili na mwanaharakati wa kijamii, ambaye anakumbuka kukutana nao katika maharusi na mazishi kabla ya mwaka 2011.

Wadah al-Keesh

Mapinduzi yalipofanyika, watu wengi katika mji wa Tarhuna walisalia kuwa watiifu kwa Gaddafi.

Koingozi huyo wa kiimla aliupendelea sana mji huo, kwa kuwapatia wanaume kutoka familia kubwa kazi nzuri katika vikosi vyake vya usalama.

Familia ya Kani ilikuwa miongoni mwa watu wachache waliounga mkono mapinduzi – lakini sio kwa maslahi ya wananchi, anasema Hamza Dila’ab, bali ni kutokana na uhasama wa miaka 30 kati yao na ndugu wa familia ya wafuasi wa Gaddafi.

Baada ya kung’olewa madarakani kwa Gaddafi, ndugu hao walipata nafasi ya kutekeleza maovu yao.

” Ndugu wa Kani walifanikiwa kuua familia hiyo kisiri mmoja baada ya mwingine ,” anasema Hamza Dila’ab.

Lakini msururu huo wa mauaji ya kulipiza kisasi ilichangia kuawa kwa ndugu mdogo wa Kani, aliyefahamika kama Ali mwaka 2012.

“Ali alikuwa ndugu mdogo mtanashati wa Kani, na alipofariki,alimfanya shujaa,”anasema Jalel Harchaoui, mtaalamu wa Libya katika taasisi ya Clingendael nchini Uholanzi, ambaye alifanya utafiti wa historia ya familia hiyo.

Three of the brothers
Maelezo ya picha,

Mohammed al-Kani,Salafist (kushoto),na wauaji wengine wawili wakuu ni, Mohsen na Abdul-Rahim

1px transparent line

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *