img

Democrats wachukua udhibiti wa bunge la seneti kupitia ushindi wa Warnock na Ossoff

January 7, 2021

Chama cha Democrat cha rais mteule Joe Biden sasa kina udhibiti wa mabunge yote mawili ya Marekani baada ya kuibuka na ushindi wa viti viwili vya Seneti.

Democrat kimenyakua viti hivyo katika uchaguzi wa marudio jimbo la Georgia. Viti hivyo vilikuwa chini ya mahasimu wao chama cha Republican muhula uliopita.

Hili ni pigo kubwa la kisiasa kwa rais anayeondoka madarakani Donald Trump wa Republican.

Kwa mara ya kwanza toka mwaka 2009 chama cha Democrat kitakuwa na udhibiti wa Ikulu ya White House, Bunge la Wawakilishi (Congress) na Bunge la Juu (Seneti).

Takriban watu milioni nne walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa marudio jimboni Georgia.

Uchaguzi huo wa Maseneta ulilazimika kurejewa kwa kuwa hakuna aliyefikia asilimia 50 ya kura ulipofanyika uchaguzi mkuu Novemba 2020.

Sasa Raphael Warnock na Jon Ossoff wamewashinda Maseneta waliokuwa wakitetea viti vyao Kelly Loeffler na David Perdue.

Bwana Warnock, ambaye ni mchungaji wa kanisa la Baptist, anakuwa seneta wa kwanza mweusi wa Georgia, jimbo ambalo Liliingia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani ikitaka utumwa uendelee.

Pia anakuwa seneta wa 11 mweusi katika historia ya Marekani.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *