img

Capitol siege: Uvamizi wa bunge unamaanisha nini kwa utawala wa Trump

January 7, 2021

Dakika 10 zilizopita

Donald Trump at rally in front of White House

Hivi ndivyo urais wa Trump unavyokamilika kwa kishindo.

Kwa wiki kadhaa, Donald Trump amekuwa akitaja Januari 6 kama siku ya masiku. Ilikuwa siku ambayo aliwaambia wafuasi wake kuja Washington DC, na kushinikiza Congress – na Makamu wa Rais Mike Pence – kupuzilia mbali matokeo ya uchaguzi mkuu wa Novemba na kuacha urais mikononi mwake.

Jumatano asubuhi, rais na wazungumzaji wanzake waliwacha gari.

Wakili wa kibinafsi Bw. Trump Rudy Giuliani, alisema mezzo wa uchaguzi utasuluhishwa kupitia “mapigano”.

Donald Trump Jr, mwana mkubwa wa rais alikuwa na jumbe kwa wafuasi wa chama chake ambao “hawatampigania” rais wao.

“Chama cha Republican sio chao tena,” alisema. “Hiki ni chama cha Republican cha Donald Trump.”

Alafu rais mwenyewe akazidi kuhamasisha vurugu kwa kundi la watu ambalo lilizidi kuongezeka na kuimba kwa nguvu “komesheni wizi” na “upuzi” huku rais akiwashawishi kutembea kutoka White House hadi bungeni Katina jengo la Capitol Hill.

“Hatutarudi nyuma. Hatutakubali,” rais alisema. “Nchi yetu haitakubali tena. Hatuwezi kuvumilia tena.”

Section divider

Rais alipokuwa anakamailisha kauli yake, sarakasi nyingine ilikuwa inaendelea ndani ya bunge, wakati wa kikao cha pamoja cha kujumuisha matokeo ya kura ya wajumbe kutoka majimbo yote.

Kwanza, Pence – alipuuzia ombi la rais la kurudia matokeo ya uchaguzi kutoka majimbo yaliyozozaniwa – na kutoa taarifa kwamba hana mamlaka ya kufanya hivyo akiongeza kuwa jukumu lake “kwa kiasi kikubwa ni la kisherehe”.

Kisha Warepublican wakawasilisha ombi la kupinga, kura za Arizona, ambapo bunge la wawakilishi na lile la seneti zilitengana na kuanzanza majadiliano ikiwa zikubali ushindi wa Joe Biden katika jumbo hilo.

Vikao bungeni vilendelea kwa utaratibu huku pande zote mbili zikishanggilia maspika wao wakitoa tamko.

“Kiapo nilichokula Jumapili iliyopita kutetea na kuunga mkono Katiba kinanifanya niwajibike kupinga uovu huu,”alisema mbunge mpya Lauren Boebert, ambaye aligonga vichwa vya habari aliposisitiza kuwa ataingia bungeni akiwa na bunduki. “Sitakubali watu wapuuzwe.”

Protesters outside the Capitol

Ndani ya seneti,mjadala ulichukua mkondo mwingine. Kiongozi wa wengi katika bunge la Seneti Mitch McConnell, aliyekuwa amevalia suit nyeusi sawa na ya kwenda mazishini, alikuwa amekuja kumzika Donald Trump, sio kumsifu.

“Ikiwa huu uchaguzi ungelifutwa kutokana na made ya upend ulioshindwa, demokrasia yetu ingelikuwa imeingia mzunguko wa kifo,” McConnell alisema. ” atungeliona tena nchi nzima ikikubali matokeo ya uchaguzi. Kila baada ya miaka minne tungelishuhudia jinsi watu wakig’ang’ania madaraka kwa gharama yoyote.”

Seneta wa Kentucky, ambaye atakuwa kiongozi wa wachache baada ya chama chake kushindwa hivi punde huko Georgia, alisema bunge lilibuniwa ” ukomesha matamanio ya muda mfupi ambayo yanaweza kuhujumu msingi wa nchi yetu”.

Matamshi yake yalikuwa bado yanagonga vichwa vya wenzake kumbe nje ya bunge hali ilikuwa imebadilika baada ya wafuasi wa Trump ambao huenda walikuwa wamehamasika na hotuba za awali, kuamua kuvamia bunge.

Waandamanaji walipambana na maafisa wachache wa usalama waliyokuwa langoni na kungia ndani ya bunge. Vikao vilisitishwa ghafla huku wabunge, wafanyakazi wa bunge na wanahabari wakilazimika kujificha kwa kuhofia usalama wao.

Capitol police point guns at a protester from inside the Senate chamber

Maelezo ya picha,

Maafisa wa polisi bungeni wakiotesha bunduki kwa mmoja wa waandamanaji ndani ya bunge la Seneti

Sarakasi iliendelea kushuhudiwa bungeni huku vituo vya Televisheni vikionesha picha za waandamanaji wakicheza densi katika nje la bunge huku wakipeperusha bendera.

Picha za waandamanaji waliokuwa ndani ya bunge zilianza kusambazwa katika mitandao ya kijamii, baadhi yao wakijaribu kuvunja madirisha na kuingia katika ofisi za wabunge; huku maafisa wa usalama wakiionekana wakiwaelekezea bunduki ndani ya bunge la Wawakilishi oyuma ya milango iliyokuwa imefungwa.

Section divider

Huko Wilmington, Delaware, Rais Mteule Joe Biden aliahirisha hotuba yake kuhusu masuala ya uchumi iliyokuwa imepangwa na kulaani kile ilicho kiita “uasi” mjini Washington.

“Saa hii demokrasia yetu iko chini ya shambulio lisilokuwa la kawaida tofauti na kitu chochote kile tulichokiona katika nyakati za kisasa, “alisema.” Shambulio dhidi ya ngome ya uhuru, Capitol yenyewe. “

Alikamilisha hotuba yake fupi kwa kumtaka Trump: kujitokeza katika televisheni ya kitaifa kulaani ghasia hizo “agiza kukomehswa kwa vurugu hizi”.

media captionJoe Biden: The scenes of chaos at the Capitol do not reflect a true America, do not represent who we are

Dakika cache baadaye, Trump alitoa ujumbe wake kwa taifa – lakini sio kama Biden alivyopendekeza .

Badala yake, alijumuisha malalamiko yake kuhusu madai kura “kuibwa”,aliwaambia wafuasi wake “ended nyumbani, tunawapenda, nyini ni watu maalum sana”.

President-elect Joe Biden speaks amid protests in Washington

Section divider

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *