img

Azam FC kukipiga na Mlandege FC katika mashindano ya kombe la Mapinduzi

January 7, 2021

 TIMU ya AZAM FC inatarajia kucheza leo uwanja wa Aman mjini Unguja dhidi ya

Mlandege FC katika mashindano ya kombe la Mapinduzi.

Katika mashindano hayo timu ya Simba SC inatarajia kucheza kesho dhidi

ya Chipukizi saa 10 jioni huku Yanga FC ikicheza na Namungo saa

mbili usiku.

Timu ya Mtibwa Sugar ambao ni mabingwa watetezi wa mashindano hayo

ya kombe la Mapinduzi imeanza vyema jitihada zake za kutwaa tena kombe hilo

baada ya juzi kuifunga Chipukizi bao 1-0 ndani ya dakika 57.

Mchezo huo ulichezwa kwenye dimba la Amaan majira ya saa 10:00 jioni ambao

ulihudhuriwa na mashabiki kiasi ambapo licha ya kushinda mechi hiyo Mtibwa

wilipata upinzani mkali kutoka kwa timu ya Chipukizi.

Timu hizo zilikianza kipindi cha kwanza kwa kushambuliana kwa zamu kila

mmoja akisaka bao la kuongoza, lakini hadi kipindi cha kwanza kinamalizika

hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwezake.

Katika kipindi cha pili timu ya Mtibwa Sugar ilianza kulishambulia lango

la Chipukizi huku ikifanya mabadiliko ya kumtoa Salum Kanoni na kumuingiza  

Ibrahim Hilika dakika ya 54.

Mabadiliko hayo yalileta neema kwa Mtibwa ambapo dakika ya 57 Mtibwa

ilijipatia bao hilo pekee lililotiwa kimiani  na Ibrahim Hilika.

Katika dakika ya 60 timu ya Chipukizi nayo ilifanya mabadiliko kwa kumtoa

mchezaji Ali Khamis na kumuingiza Mundhir  Iman, ili kuongeza kasi ya

mashambulizi kwa kutafuta bao la kusawazisha lakini walishindwa kutumia

nafasi walizozipata.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *