img

Watu watatu wamekufa baada ya mashua kuzama ziwa Kivu

January 6, 2021

 

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo watu 3 wamekufa katika ajali mpya baada ya boti kuzama usiku wa kuamkia leo kwenye ziwa Kivu. 

Hadi mapema leo asubui, watu 56 wameokolewa wakiwa hai. Shirika la kiraia la Kalehe limesema watu wengine zaidi ya 20 bado hawajaonekana. 

Boti hiyo ilikuwa inatokea katika kijiji cha Luhihi kilicho katika eneo la Kabare mkoani Kivu kusini hapo jana jioni, na ikielekea Goma katika mkoa wa Kivu kaskazini. 

Ilizama saa chache baadae katika kijiji cha Nyabirehe wilaya jirani ya Kalehe, Kivu kusini. Viongozi wa mkoa wa kivu kusini wameeleza kwamba boti hiyo iliwabeba abiria 60 pekee, na kwamba ajali hiyo ilisababishwa na dhoruba kali iliyokuwepo usiku huo. 

Shirika la kiraia huko Kalehe limelaumu hali mbaya ya vyombo vya usafirishaji vinavyotumiwa na wakaazi wa visiwa vya ziwa Kivu.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *