img

Virusi vya corona: Wachunguzi wa corona wa WHO wazuiliwa kuingia China

January 6, 2021

Dakika 9 zilizopita

Vendors are selling fish in an open market in Wuhan, Hubei province, China, 2 December 2020

Wanachama wawili tayari walikuwa safarini kuelekea China, huku WHO ikisema tatizo ni ukosefu wa kuidhinshwa kwa visa.

Hata hivyo, China imepinga madai hayo, ikisema kuwa maelezo kuhusu ziara hiyo ikiwa ni pamoja tarehe, bado inapangwa.

Uchunguzi huo ulikuwa ufanyike baada ya Beijing kuitikia ombi la miezi kadhaa kutoka WHO.

Virusi vya corona viligunduliwa kwanza Wuhan mwisho wa mwaka 2019, mlipuko wa kwanza ukihusishwa na soko la nyama katika eneo hilo mji huo.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa “amesikitika sana ” kwamba China haijakamilisha idhini ya maafisa hao kuingia nchini humo “ikizingatiwa kuwa maafisa wawili tayari wameanza safari na wengine walishindwa kusafiri dakika za mwisho”.

“Nilihakikishiwa kwamba China inaharakisha kukamilisha mchakato wa ndani kwa maafisa hao,” aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva siku ya Jumanne, akielezea kwamba amekuwa akiwasiliana na maofisa wa ngazi ya juu wa China akisisitiza kuwa “mpango huo ni muhimu kwa WHO na ulimwengu kwa ujumla”.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Hua Chunying ameiambia BBC “huenda kulitokea na mkanganyiko wa mawasiliano” na kwamba “hakuna haja ya kuendeleza uchumi usiokuwa na msingi”.

“Mamlaka za China zinashirikiana kwa karibu na WHO lakini kumekuwa na milipuko wa virusi katika maeneo tofauti duniani na nchi nyingi zimekuwa zikijizatiti kuzuia kuenea kwa virusi na sisi pia tunakabiliwa na hali hiyo,” alisema.

“Bado tunaunga mkono ushirikiano wa kimataifa na kuendeleza mkakati wa ndani wa kukabiliana na jana hilo.

Tumekuwa tukiwasiliana na WHO na kufikia sasa nafahamu kuwa tarehe ya ziara hiyo na mipango mingine bado inajadiliwa.”

WHO imekuwa ikijiandaa kuwapeleka wataalamu 10 wa kimataifa China kwa miezi kadhaa kwa lengo la kuchunguza chimbuko la janga la corona na ni lini virusi vilivyotoka kwa wanyama na kuingia binadamu.

Mwezi uliopita shirika hilo lilitangaza kuwa uchunguzi huo utaanza mwezi Januari mwaka 2021.

Baadhi ya tafiti zinaashiria kuwa virusi vya corona vinavyoweza kuambukizwa binadamu huenda vimekuwa vikisambazwa na popo bila kujulikana kwa miongo kadhaa.

Hata hivyo haijabainika ni nani aliyepata virusi hivyo kwanza kati ya pope na binadamu.Kundi la maafisa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) lililokuwa lichunguze chanzo cha Covid-19 katika mji wa Wuhan limezuiliwa kuingia China.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *