img

Tuzo za Grammy zaahirishwa

January 6, 2021

Tuzo za Grammy za mwaka 2021 hazitafanyika tena mwezi huu huko Los Angeles California na badala yake zitatangazwa mwezi Machi kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vya virusi vya corona na vifo.

Waandaji wa tuzo hizo waliwaambia jana Jumanne kuwa onyesho la kila mwaka litasogezwa mbele kutoka tarehe yake ya awali ya Januari 31 hadi tarehe isiyojulikana mwezi Machi.

Tuzo hizo za Grammy zitafanyika Los Angeles katika Kituo cha Staples, Kaunti ya Los Angeles, ambako ndio kitovu cha ugonjwa huko California, ambako umezidi vifo 10,000 na imekuwa na asilimia 40 ya vifo.

Beyonce ndiye anayeongoza katika tuzo hizo mwaka huu akiwa na uteuzi katika vitengo tisa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *