img

Qatar kuondolewa marufuku na nchi za Kiarabu kunamaanisha nini?

January 6, 2021

Dakika 12 zilizopita

El emir de Qatar Tamim Al Thani y el príncipe saudita Mohammed bin Salman.

Mzozo wa kidiplomasia kati ya Qatar na mataifa ya jirani ya ghuba ya wajemi, ambayo yaliilaumu kwa kuunga mkono ugaidi, hatimaye umekomeshwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Siku ya Jumatatu, Saudi Arabia ilifungua mipaka yake ya majini, ardhini na angani kwa Qatar, ambayo ilikuwa imefungwa tangu Juni 5, 2017, wakati Saudia, Umoja wa falme za kiarabu, Bahrain na Misri zilipovunja uhusiano wa kidiplomasia na Doha.

Na Jumanne, mkataba wa kumaliza mzozo huo ulitiwa saini katika mji wa Saudia wa el-Ula, wakati wa kongamano la Baraza la Ushirikiano la Ghuba Cooperation (GCC) ambalo pia litahudhuriwa na Emir wa Qatar.

Líderes

Kulingana mwandishi wa BBC Lyse Doucet, chanzo kilichohusika katika kupanga kongamano hilo kilisema hatua ya Saudia kufungua anga zake na mipaka ya ardhini na majini ililenga kumsaidia kujenga imani ya kumhakikishia Emir Tamim bin.

Hamad Al Than alisema kila kitu ni shwarii.

Mwaka 2017, wakati vikwazo vilipowekwa, kiongozi huyo wa Qatar alisema hatasafiri katika nchi yoyote ambayo itawazuia watu wa nchi yake kuingia.

Japo vikwazo hivyo vya usafiri vya miaka mitatu na nusu viliathiri jana ucumi wa Qatar, lakini pia viliathiri mshikamano na umoja wa nchi wa za Ghuba.

Hali hiyo imechangiwa na mabadiliko katika mazingira ya siasa za kimataifa.

Kongamano la GCC sasa litaanzisha mchakato wa kuimarisha uhusiano ambao ulikuwa umedorora.

Doha

Bila shaka, kama anavyoeleza mwandishi wa BBC wa masuala ya usalama Frank Gardner, “kuondolewa kwa marufuku dhidi ya Qatar kulihitaji subira na diplomasia ya hali ya juu, hususan upande wa Kuwait, lakini pia kutokana na shinikizo la hark kutoka kwa serikali.

White House pia ilichangia ikizingatiwa kuwa utawala Trump unaondoka madarakani. “

Profesa wa Chuo Kikuu cha Kuwait Bader al-Saif, haha hive amepuuzilia mbali jukumu la utawala wa Trump katika kukomeshwa kwa mzozo huo, akiandika kwenye Twitter kwamba licha ya Marekani kuwa sehemu ya suluhisho, pia ilikuwa “sehemu ya tatizo” kwa kuifurisha kichwa Saudi Arabia kutokana na msaada bila masharti.

Kwa upande wake, Karen Young, mtaalamu wa siasa ya uchumi wa Ghuba kutoka taasisi ya American Enterprise, alitoa maoni yake katika taarifa iliyonukuliwa na Gazeti la The Guardian akisema kuwa makubaliano hayo yamechangiwa pakubwa na mabadiliko yanayokuja Washington na kujitathmini upya, “kwa maslahi tofauti ya nchi wanachama wa GCC.”

Kwa Young, nchi zingine za Ghuba zinahitaji Qatar katika “hema” ya GCC, lakini hiyo haimaanishi wana mtazamo mmoja kuhusu jukumu lake katika eneo hilo.

Maoni ambayo Gardner pia anakumbaliana nayo: ni onyo kwamba Qatar “haitasamehe wala kusahau kile ambacho inachukulia kuwa hujuma kutoka kwa majirajni zake wa Ghuba ya Uajemi.”

“Kando na masala ya kidiplomasia, nchi moja hususan, Umoja wa Falme za Kiarabu, inatilia shaka ikiwa Qatar itabadilisha miendendo yake.

mm

Japo Qatar imepinga kuunga mkono ugaidi, imekuwa ikiunga mkono vuguvugu la Kiislamu la kisiasa huko Gaza, Libya na maeneo mengine hasa Muslim Brotherhood, ambayo UAE inachukulia kuwa tisho kwa utawala wake, “anaeleza mtaalamu wa BBC.

“Hata hivyo, kuondolewa kwa marufuku hiyo kumeileta Qatar karibu na Saudia ambayo imekuwa adui kinadharia kwa: Uturuki na Iran,” aliongeza.

Ukweli ni kwamba vikwazo viliwekwa baada ya Qatar kukataa kutekeleza msururu wa masharti yaliyojumuisha kufungwa kwa televisheni ya Al Jazeera na kukomesha uhusiano wake wa kidiplomasia na Iran, ambayo haijafanyika.

Na kwa sasa, makubaliano ya Qatar inaonekana kuondoa kesi iliyokuwa imewasilisha mahakamani dhidi ya Saudi Arabia na washirika wake wa Ghuba.

Kumaanisha, katika mazingira yoyote, kuondolewa kwa marufuku ni hatua ya kwanza katika mchakato wa muda mrefu ambao hauwezi kuzuia kutokea kwa mzozo mwingi.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *