img

Mwili wa Rosemary Nyerere kuzikwa leo Dar

January 6, 2021

Mwili wa mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rosemary Nyerere, unatarajiwa kuzikwa leo Januari 6, katika Kituo cha Hija kilichopo Pugu jijini Dar es Salaam.

Mazishi ya Rosemary Nyerere, mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere yanatarajiwa kufanyika Jumatano ya Januari 6 katika Kituo cha Hija kilichopo Pugu jijini Dar es Salaam.

Eneo hilo huzikwa wafia dini ambao kwa mujibu wa familia, wamesema alichagua Rose mwenyewe wakati wa uhai wake.

Msemaji wa familia, Bhoke Nyerere amesema, Rose wakati wa uhai wake alichagua azikwe katika eneo hilo.

“Mama yangu mdogo alijiunga na Shirika la Ufransicam na wakati wa uhai wake aliomba atakapofariki azikwe pale kwenye eneo ambalo wanazikwa wafia dini,” anasema.

Msiba upo Mikocheni, nyumbani kwa Mwalimu Nyerere ambako familia na waombolezaji wengine wamekusanyika kwa ajili ya kuomboleza msiba huo.

Kuhusu taratibu nyingine alisema Jumatano kutakuwa na ibada fupi nyumbani kabla ya kuelekea katika Kanisa la Mtakatifu Imaculata lilipo Upanga ambapo ibada ya maziko itafanyika.

Bhoke amesema baada ya ibada hiyo msafara utaelekea moja kwa moja Pugu kituo cha mahujaji kwa ajili ya maziko.

Rosemary ambaye ni mmoja kati ya watoto saba wa Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere alifariki dunia jioni ya Januari Mosi, 2021 katika hospitali ya Mzena Kijitonyama alikokuwa akipatiwa matibabu.

Hata hivyo hadi sasa haijawekwa wazi sababu ya kifo cha Rose, hata msemaji wa familia alipoulizwa kuhusu hilo alijibu kwamba anayeweza kuzungumzia ni daktari.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *