img

Mtibwa Sugar yapania kufanya vizuri kombe la Mapinduzi

January 6, 2021

 

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umeweka wazi kwamba utafanya vizuri kwenye Kombe la Mapinduzi kwa msimu huu wa 2021 kwa kuwa umejipanga kufanya hivyo.

Mtibwa Sugar ni mabingwa watetezi walianza vizuri jana, anuari 5 kwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chipukizi kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Bao la ushindi lilifungwa na Ibrahim Hilika na kuifanya timu hiyo kuibuka mashujaa ndani ya dakika 90 mbele ya wapinzani wao.

Kocha wa Mtibwa Sugar, Vincent Barnaba amesema kuwa mwanzo ambao wameanza nao unawafanya waamini kwamba watafanya vizuri kwenye mechi zao zijazo na kuweza kutetea taji hilo.

“Tupo vizuri na ninaona kwamba wachezaji wanapambana ndani ya uwanja kupata matokeo, kila mmoja anapambana kufanya vizuri hivyo mashabiki wazidi kutupa sapoti.

“Imani yetu ni kuona kwamba tunaweza kufikia malengo ambayo tumejiwekea, mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Ubingwa waliotwaa msimu wa 2020 kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba ni wa pili kwa timu hiyo yenye maskani yake pale Morogoro.

Ikiwa itatwaa tena msimu huu wa 2021 itakuwa ni mara yao ya tatu kutwaa na itakuwa sawa na Simba ambao nao pia wametwaa mara tatu.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *