img

Mfanyabiashara mkubwa China ahukumiwa kunyongwa

January 6, 2021

Mfanyabiashara mkubwa wa China ambaye pia ni amewahi kuwa Kiongozi wa Chama, Lai Xiaomin amehukumiwa kunyongwa baada ya kukutwa na hatia ya Rushwa ya takriban Tsh. Bilioni 643.

Mahakama imesema alijihusisha na vitendo vya Rushwa kwa miaka 10 tangu mwaka 2008 ambapo alikuwa anapokea fedha ili kuwapa watu Ajira, kuwapandisha madaraja au kuingia mikataba.

Lai alianza kuchunguzwa mwaka 2018 ambapo pia alifukuzwa uanachama wa Communist Party of China. Kwa mujibu wa Shirika la Amnesty International, Nchi hiyo inanyonga watu wengi kuliko nyingine yoyote duniani.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *