img

Kampuni za China zapigwa marufuku kufanya biashara Marekani ikiwemo ya Jack Ma

January 6, 2021

Rais wa Marekani Donald Trump amesaini amri ya rais ya kupiga marufuku kampuni nane za China zenye program ya kutoa huduma ya ulipiaji wa bidhaa kwa njia ya mtandao.

Programu hizo ni pamoja na ile maarufu ya mtandao wa Alipay inayomilikuwa na mfanyabiashara tajiri China Jack Ma, QQ Wallet na WeChat pay.

Amri hiyo inaanza kutekelezwa ndani ya siku 45 baada yar ais kusema kuwa programu hizo zinapigwa marufuku kwasababu ni tishio kwa usalama wa taifa la Marekani.

Inasemekana kuwa kuna uwezekano program hizo zinatumika kufuatilia na kupata data za raia wa Marekani.

Programu zingine zilizopigwa marufuku ni pamoja na Tencent QQ, CamScanner, SHAREit, VMate na WPS Office.

“Marekani lazima ichukue hatua madhubuti dhidi ya waliotengeneza na kudhibiti programu za China kulinda usalama wa taifa letu,” Amri hiyo ya rais imesema.

Aidha, amri hiyo ya Rais Trump inasema “kwa kufikia bidhaa za elektroniki za simu aina ya smartphones, tablets, na kompyuta, programu za China zinaweza kufikia taarifa muhimu za watumiaji ikiwemo taarifa nyeti za utambulisho na taarifa za kibinafsi.”

Utawala wa Trump umeongeza shinikizo kwa makampuni ya China mwezi wake wa mwisho madarakani ikiwemo kampuni anazozichukulia kuwa zenye kuhatarisha usalama wa taifa hilo.

Rais Trump amesaini amri kadhaa za rais dhidi ya kampuni za China kwa madai kwamba huenda zikashirikisha data za raia wa Marekani kwa serikali ya China.

media captionAmbar, an influencer, say she has seen inappropriate content on TikTok

Chinese social media app TikTok and telecoms giant Huawei have been among the casualties of Washington’s crackdown.

Mwezi uliopita, Wizara ya biashara iliongeza kampuni kadhaa za China ikiwemo ya kutengeneza chipu ya SMIC na ndege zisizo na rubani ya DJI Technology kwenye orodha ya zilizopigwa marufuku kufanya biashara.

Utawala wa Trump pia uliweka masharti kwa makapuni ya China na Urusi kwa madai ya kushirikiana kijeshi na kununua bidhaa nyeti pamoja na teknolojia za Marekani.

China imekanusha mara kadhaa madai kuwa kampuni za nchi yake zinaishirikisha data walizonazo za raia wa Marekani na imejibu madai hayo kwa kuweka masharti makali kwa kampuni za China zinazofanya manunuzi nje ya nchi hiyo kwa kupiga marufuku ununuaji wa teknolojia ya kijeshi.

Agosti mwaka jana, Marekani iliagiza kampuni ya ByteDance, inayomiliki mtandao wa kijamii wa programu ya TikTok, ama ifunge mtandao huo au iuze mali zake zilizopo Marekani.

Licha ya kushindwa kutekeleza mauzo yake kwa siku ya mwisho iliyokuwa imewekwa, Marekani bado haijafunga programu hiyo na inaendeleza mazungumzo ya utendani kazi wa kumpuni hiyo siku za baadaye.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *