img

Dk Shein afungua chuo cha utalii

January 6, 2021

RAIS  mstaafu wa Zanzibar awamu ya saba Dk. Ali Mohammed Shein amesema umefika wakati wa kufanya mabadiliko ya kutolewa mafunzo  yatayoendana na wakati ili kuweza kupanua wigo wa soko la ajira nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa jengo la Chuo cha Utalii huko Maruhubi  ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra ya kutimiza miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Dk,Shein amesema imefika wakati wa  wanafunzi wanaosoma chuo cha utalii kupatiwa  mafunzo yanayoendana na wakati ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira katika sekta ya utalii .

Amewashauri wanafunzi wa chuo hicho kusoma kada tofauti za sekta utalii ambayo imekuwa tegemeo kubwa la vijana wengi kupata ajira hivi sasa nchini.            

Vilevile Dk Shein amesema ni vyema kuzalishwa vijana wenye taaluma stahiki kwa kuendelezwa  vivutio vilivyopo kwa kufuatwa mila  silka na tamaduni za nchi .

Amesema maendeleo yanayopatikana ni miongonii mwa sekta  ya utalii nchini kwa kuwepo kwa vyanzo tofauti vya utalii zikiwemo hoteli zenye sifa.

Hata hivyo amesisitiza kutunzwa kwa chuo hicho kiwe katika mazingira safi  ili kiweze kidumu kwa muda mrefu kutokana na gharama kubwa zilizotumika na serikali katika ujenzi wa jengo hilo ambalo lenye lengo la kuzalisha wataalamu wa fani tofauti katika sekta ya utalii ambayo ni tegemeo kubwa katika uingizaji wa pato la uchumi wa nchi.

Mapema Waziri wa Elimu wa Mafunzo  ya Amali  Simai Mohammed Said ameahidi kuendelea kutafuta masomo wafanyakazi wa  Chuo cha Utalii katika nchi tofauti ili vijana waweze kutumia fursa yakwenda kujifunza kuendesha harakati za kiutalii kiutaalamu zaidi.

Amesema sekta ya utalii imekuwa ikichangia pato kubwa kwa nchi ,hivyo kufanya hivyo kutaweza kuwapatia nafasi zaidi za ajira vijana.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu  na Mafunzo ya Amali Dk Idrisa Muslim Hijja amesema lengo la ujenzi huo ni kuzalisha wataalamu ili kuongeza nafasi za ajira kwa vijana katika kukabiliana na  tatizo la ukosefu wa ajira nchini.

Jengo hilo la ghorofa mbili  lina jumla ya madarasa matano vyumba tisa vya kulala limegharimu  bilioni  5.66 na limefadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB)

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *