img

COVID-19- Senegal yatangaza hali ya dharura kwa mara ya pili

January 6, 2021

Rais wa Senegal Macky Sall hapo jana alitangaza hali mpya ya dharura kutokana na kuongezeka kwa idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona katika maeneo mengi ya taiga hilo la Afrika Magharibi. 

Kuanzia hii leo, marufuku ya kutotoka nje nyakati ya usiku itaanza kuzingatiwa katika miji ya Dakar na Thies, ambayo Sall amesema ndiyo yenye asilimia 90 ya maambukizi hayo.

 Kuvaa barakoa ni lazima kwa kila mtu na mikusanyiko ya watu wengi pia imepigwa marufuku. Masharti hayo mapya yametangazwa baada ya maisha kuruhusiwa kurudi katika hali ya kawaida ili kufufua uchumi uliozoroto kufuatia hali ya dharura iliyotangazwa wakati wa wimbi la kwanza la maambukizi hayo ya ugonjwa wa COVID-19. Mnamo Desemba 26, idadi ya maambukizi iliongezeka hadi watu 240. 

Na desemba 29, vifo saba viliripotiwa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *