img

Barcelona yapokea majibu ya Covid-19

January 6, 2021

Baada ya maafisa wawili wa Barcelona kuripotiwa na Covid-19 usiku wa jumatatu na kupelekea kambi ya mazoezi ya klabu hiyo kufungwa kwa muda, hii leo majibu ya vipimo vya Covid-19 vimetoka na kuonesha wachezaji wa wote wa Barcelona hawana Covid-19.

Ripoti ya maafisa wawili kuwa na Covid-19 ilizua hofu huenda baadhi ya wachezaji wa Barcelona wangekuwa na ugonjwa huo hivyo kupelekea mchezo wao dhidi ya Athletic Bilbao wa La Liga kuwa na hati hati ya kughairishwa lakini kutokana na majibu hayo mchezo huo unatazamiwa kucheza leo.

Barcelona watakuwa ugenini kukipiga dhidi ya Athletic Bilbao kwenye dimba la San Mames mishale ya saa 5:00 usiku wa leo Januari 6 na kufukuzia ushindi ili kuweka hai matumaini yao ya kufukuzia ubingwa wa ligi hiyo.

Kuelekea kwenye mchezo huo, wenyeji Bilbao ambao siku mbili zilizopita wamemtambulisha Marcelino Garcia kuwa kocha wao mpya, huenda Alex Berenguer na Iker Muniani wakarejea kikosini baada ya kuwa hawana nafasi za kudumu kutokana na mfumo wa kocha aliyepita Garitano.

Kwa upande wa Barcelona wanataraji Miralem Pjanic, Francisco Trincao na Antoinne Greizmann kurejea kikosini na kuchagiza wakali hao wa Catalunya kuendeleza wimbi na kutofungwa baada ya kucheza michezo 6 ya La Liga bila kupoteza hata mmoja.

Barcelona ambayo ndiyo timu inayoongoza kwa ufungaji mabao, mabao 30 kwenye msimamo wa La Liga inashika nafasi ya 5 ikiwa na alama 28 wakati Bilbao wanashika nafasi ya 9 wakiwa na alama 21.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *