img

Watalaamu wa WHO kwenda China kuchunguza chanzo cha corona

January 5, 2021

 

Ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kutokea mripuko wa virusi vya corona, wataalamu wa Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO wanatarajiwa kuwasili China kwa ajili ya uchunguzi wa vyanzo vya kirusi hicho. 

China ilichelewesha kuidhinisha ziara ya watalaamu wa kimataifa nchini humo kufanya uchunguzi wa vyanzo vya janga hilo, hatua iliyozusha tuhuma za kutaka kuficha ukweli pamoja na kula njama na kuwepo hofu ya kufanya udanganyifu. 

Lakini WHO sasa imesema China imetoa ruhusa kwa watalaamu wake kuzuru nchi hiyo. Timu hiyo ya watu 10 inatarajiwa kuwasili nchini humo muda mfupi ujao kwa ziara ya wiki tano au sita, ikiwa ni pamoja na kujiweka karantini kwa wiki mbili. 

Maafisa wa China wamekataa kuthibitisha tarehe kamili za maelezo ya ziara hiyo, katika kile kinachoashiria unyeti wa ujumbe huo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *