img

Virusi vya corona: Uingereza,Scotland waanza marufuku mpya ya kutotoka nje

January 5, 2021

Dakika 5 zilizopita

Boris Johnson speaks at Downing Street

Uingereza na maeneo mengi ya Scotland yameweka marufuku mapya ya kuwataka watu wasitoke nyumbani kwao.

Shule zimefungwa tena nchini Uingereza, Scotland na Wales, wakati Northern Ireland itaongeza muda kusoma wakiwa nyumbani.

Sheria za Uingereza zinatakiwa kupitiwa upya mnamo Februari 15; Scotland itapitia sheria yake mwishoni mwa Januari.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoa angalizo kuwa wiki zijazo hali itakuwa ngumu.

Wakati huohuo , Kansela Rishi Sunak ametangaza kuwa wafanya biashara wa bidhaa za rejareja pamoja na wafanyakazi wa hotelini na sehemu za mapumziko watapewa ruzuku ya mara moja yenye thamani ya hadi Pauni 9,000, na kipimo kilichotengwa kikiwa ni Pauni bilioni 4 katika maeneo yote ya Uingereza.

Na waziri Michael Gove amethibitisha kuwa mitihani ya sekondari itafutwa mwaka huu, na wizara itahakikisha kuwa wanafunzi wanapimwa uwezo wao bila upendeleo wowote.

Hatua hii inakuja baada ya Uingereza kuripoti kuwa na maambukizi 58,784 siku ya Jumatatu pamoja na idadi ya vifo kuongezeka na kufika 407 ndani ya siku ya siku 28 .

Wakati waziri mkuu akitangaza marufuku ya kutoka nje, bwana Johnson alisema hospitali zina msukumo mkubwa wa Covid kuliko wakati mwingine wowote tangu janga hili lianze”.

A woman wearing a face mask walks past a coronavirus poster in Glasgow

Ametoa agizo la watu kukaa ndani na kutoka tu pale inapowabidi kwa ajili ya mahitaji maalum kama – dawa na chakula, mazoezi na kazi zinaweza kufanyika watu wakiwa nyumbani- shule na vyuo inabidi vifundishe mtandaoni.

Na alisema nyumba za malezi na wahudumu wao na kila mtu mwenye zaidi ya miaka 70 , wafanyakazi wa afya watapewa kipaumbele kupata chajo mpaka ifikapo katikati ya mwezi Februari.

Wakati maagizo yanakuwa sheria mapema asubuhi ya Jumatano, watu wanapaswa kuzifuata, waziri mkuu aliongeza.

Mapema Jumatatu, waziri wa Nicola Sturgeon alitoa agizo la watu kutotoka nyumbani huko Scotland, wameanza marufuku hiyo usiku wa leo na itaendelea mpaka Januari mwishoni.

Maeneo ya kuabudu, shule zitafungwa na mikusanyiko ya watu imepigwa marufuku.

” si kama ninakuza mambo ila ninahofia hali ile ambayo ilitokea mwezi Machi mwaka jana,” Sturgeon alisema.

Wales, imefungwa tangu Desemba 20, shule na vyuo vitafungwa mpaka Januari 18 kwa wanafunzi wengi.

Lockdown in Newark-on-Trent

Northern Ireland, imeongeza muda wa agizo la watu kukaa nyumbani kwa muda wa wiki sita na Desemba 26, walikuwa na mpango wa kuweka agizo kuwa sheria na kuongeza mda wa wanafunzi kusoma mtandaoni.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *