img

Uingereza,Scotland waanza marufuku mpya ya kutotoka nje

January 5, 2021

Uingereza na maeneo mengi ya Scotland yameweka marufuku mapya ya kuwataka watu wasitoke nyumbani kwao.

Shule zimefungwa tena nchini Uingereza, Scotland na Wales, wakati Northern Ireland itaongeza muda kusoma wakiwa nyumbani.

Sheria za Uingereza zinatakiwa kupitiwa upya mnamo Februari 15; Scotland itapitia sheria yake mwishoni mwa Januari.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoa angalizo kuwa wiki zijazo hali itakuwa ngumu.

Wakati huohuo , Kansela Rishi Sunak ametangaza kuwa wafanya biashara wa bidhaa za rejareja pamoja na wafanyakazi wa hotelini na sehemu za mapumziko watapewa ruzuku ya mara moja yenye thamani ya hadi Pauni 9,000, na kipimo kilichotengwa kikiwa ni Pauni bilioni 4 katika maeneo yote ya Uingereza.

Na waziri Michael Gove amethibitisha kuwa mitihani ya sekondari itafutwa mwaka huu, na wizara itahakikisha kuwa wanafunzi wanapimwa uwezo wao bila upendeleo wowote.

Hatua hii inakuja baada ya Uingereza kuripoti kuwa na maambukizi 58,784 siku ya Jumatatu pamoja na idadi ya vifo kuongezeka na kufika 407 ndani ya siku ya siku 28 .

Wakati waziri mkuu akitangaza marufuku ya kutoka nje, bwana Johnson alisema hospitali zina msukumo mkubwa wa Covid kuliko wakati mwingine wowote tangu janga hili lianze”.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *