img

Tetesi za soka kimataifa

January 5, 2021

 Manchester City wanachunguza hali ya beki Sergio Ramos katika klabu ya Real Madrid wakiwa na lengo la kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 kutoka Uhispania atakayekuwa mchezaji huru msimu huu. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 29, anatarajiwa kukataa ofa ya kwanza ya kandarasi ya Manchester City na ana wasiwasi kuhusu kasi ya klabu hiyo katika mazungumzo ya kumpatia kandarasi mpya ya miaka mitano.. (Times – subscription required)

Tottenham haiko tayari kumuuza ama kumtoa kwa mkopo kiungo wa kati wa England Dele Alli, 24, mwezi huu lakini kipa wa Argentina Paulo Gazzaniga 29 na beki wa England Danny Rose 30 wataruhusiwa kuondoka. (Sky Sports)

Chelsea iko tayari kumpatia muda zaidi kocha Frank Lampard , lakini hali hiyo inaendelea kuchunguzwa huku Thomas Tuchel , Max Allegri , Brendan Rodgers na Ralph Hasenhuttl wakifikiriwa kama wakufunzi mbadala iwapo atafutwa kazi.. (Independent)

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Andriy Shevchenko, ambaye kwa sasa ndiye kocha wa timu ya taifa ya Ukraine pia anafikiriwa kujaza pengo la Lampard iwapo atafutwa. (Le10 Sport)

Arsenal haina mpango wa kumuuza Mohamed Elneny, 28, katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari huku kukiwa na hamu kutoka klabu ya. (Football London)

Mohamed El Neny

Arsenal wameipatia klabu ya Juventus kiungo wao wa kati Mesut Ozil 32 katika wiki za hivi karibuni lakini mabingwa hao wa Itali wanamuona mchezaji wa Sweden Dejan Kulusevski ,20 kama mchezaji mwenye talanta kwa siku zijazo katika safu hiyo. (CBS Sports)

Arsenal inachunguza hali ya kiungo wa kati wa Argentina Emi Buendia lakini bado hawajawasilisha ombi rasmi la mchezaji huyo wa Norwich mwenye umri wa miaka 24(Football London)

Arsenal inachunguza uwezekano wa kutoa mchezaji na kuongeza fedha kwa Buendia , ili kujaribu kuishawishi Norwich kumuuza kiungo huyo wa kati huku wachezaji wa safu ya kati Joe Willock na Reiss Nelson wakitarajiwa kukabidhiwa Norwich. (Independent)

Buendia

Beki wa Manchester United na Argentina Marcos Rojo, 30, amefanya mazungumzo na klabu ya Boca Juniors nyumbani kwao , ijapokuwa bado hawajaafikiana kuweka kandarasi. (Mail)

Kiwango cha mchezo wa beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 26, kinaweza kuishawishi Manchester United kutotafuta beki mwengine wa kati mwezi huu. (Manchester Evening News)

Wachezaji wanaolengwa na klabu ya Barcelona ni kiungo wa kati wa Liverpool na Uhalonzi Georginio Wijnaldum, 30, beki wa kati wa Manchester City na Uhispania Eric Garcia, 19, na mshambuliaji wa Lyon na Uholanzi Memphis Depay, 26.

Lakini wanakabiliwa na upinzani mkuu kuwanyakuwa wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari na badala yake huenda wakawanasa wakiwa wachezaji huru wakati ambapo kandarasi za wachezaji wote zitakua zimekamilika. (Sky Sports)

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *