img

Shamsa kupungua kilo 25 kwa ajili ya mpenzi wake

January 5, 2021

Ni ‘headlines’ za staa wa filamu na mfanyabiashara Shamsa Ford ambaye amesema mipango yake ya mwaka huu 2021 ni kuwa na muonekano mpya ambapo amepanga kupunguza mwili ili mpenzi wake asije kumuona shangazi.

Shamsa Ford amesema anataka kufanya mazoezi na diet kwa wingi ili kupungua kilo 25 ambazo zitamsaidia kwenye afya yake na muonekano wake.

“Nime-miss kaumbo kangu, huu mwaka ni mazoezi sana na diet, nataka kukata kilo 25 na nitaweza kwa ajili ya afya yangu  pia kwa ajili ya ‘my honey’  nisije nikaonekana shangazi yake bure, 2021 muonekano mpya” ameandika Shamsa Ford

Staa mwingine aliyetawala kuhusu muonekano wake ni Wema Sepetu baada ya kupunguza shepu ya mwili wake hadi kufikia kilo 65 kutoka 95.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *