img

Mzozo wa Tigray: Ethiopia kukarabati Msikiti wa al-Najashi

January 5, 2021

Dakika 6 zilizopita

Damaged mosque

Maelezo ya picha,

Msikiti wa kale zaidi Afrika ,al-Nejashi

Serikali ya Ethiopia imeahidi kukarabati Msikiti wa kale wa uliyoharibiwa mwezi uliyopita katika mzozo uliyokumba jimbo la Tigray kaskazini mwa nchi hiyo.

Msikiti wa al-Nejashi uliripotiwa kushambuliwa kwa makombora, vitu ndani kuibwa na makaburi ya kihistoria ya viongozi wa Kiislamu kuharibiwa.

Serikali ilisema Kanisa lililoharibiwa wakati wa mzozo huo pia litakarabatiwa.

Wakazi wanaamini Msikiti wa al-Nejashi ulijengwa na Waislamu wa kwanza kuhamia Afrika enzi ya Mtume Muhammad.

Walikuwa wamekimbia mateso huko Makka na wakapewa hifadhi katika uliokuwa Ufalme wa Aksum.

Waislamu katika eneo hilo wanaamini kwamba maswahaba 15 wa Mtume Muhammad walizikwa katika makaburi yaliyoharibiwa.

Pia wanasema Msikiti huo ni wa kale zaidi Afrika, japo wengine wanaamini uko Misri.

Msikiti huohuo katika mji wa Wukro, karibu kilomita 800 (miili 500) kutoka mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Kanisa la Wakristo wa Orthodox, wa Saint Emmanuel, Pia uliharibiwa lakini hakuna maelezo yaliyotolewa.

Mwaka 2015 Shirika la misaada la Uturuki ulilizindua mradi wa kuukarabati Msikiti huo, na kuongeza kuwa lilitaka ”kuhifadi turathi” hiyo ya kale na kufanya eneo hilo kuwa kivutio cha ”Utalii wa kidini”.

al-Nejashi mosque

Msikiti huo na Kanisa lililokuwa karibu na hapo liliharibiwa wakati wa oparesheni ya kijeshi ya mwezi mmoja iliyoondoa madarakani Tigray People’s Liberation Front (TPLF) katika eneo hilo Novemba 28.

Shirika lisilo la kiserikali la Ubelgiji, linaloendesha shughuli zake Afrika, mnamo Desemba 18 liliripoti kwamba Msikiti wa al-Nejashi “ulilipuliwa kwa bomu kwanza na baadaye kuporwa na wanajeshi wa Ethiopia na Eritrea”.

” Vyanzo via habari ndani ya Tigray zinasema kwamba watu kadhaa walifariki wakijaribu kulinda Msikiti huo,” iliongezza ripoti hiyo.

Serikali haijatoa tamko lolote kuhusiana a na repoti hizo. Serikali zote za Ethiopia na Eritrea pia zinakanusha kuwa vikosi vya Eritrea viko Tigray kusaidia katika vita dhidi ya TPLF.

2px presentational grey line
Ruins of the palace of the Queen of Sheba near Axum, Aksum, Dongur Palace

Jumatatu, televisheni ya serikali ya Ethiopia ilinukuu wakazi wakisema kwamba vikosi vya TPLF vilichimba mitaro kuzunguka msikiti huo, bila kutoa maelezo zaidi.

Serikali imeweka vikwazo vikali dhidi ya vyombo vya habari kuripoti kuhusu hali ilivyo ndani ya Tigray, na kufanya kuwa vigumu kubaini ni lini vikwazo hivyo vitaondolewa.

Wafanyakazi wa kutoa misaada pia wamedhibitiwa kuingia Tigray.

Katika mahojiano na BBC Idhaa ya Amharic, Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya kuhifadhi maeneo ya kale, Abebaw Ayalew, alisema kamati maalum itapelekwa kutathmini kiwango cha uharibifu dhidi ya Msikiti na Kanisa kabla shughuli ya ukarabati kuanza .

“Maeneo haya sio ya kuabudu pekee, Bali pia ni turathi ya kale kwa Ethiopia nzima,”alisema.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *