img

Mapacha waliounganika Marieme na Ndeye wanaendelea vyema katika shule ya Cardiff

January 5, 2021

Dakika 8 zilizopita

The twins in school

“Mapacha waliounganika ambao walitarajiwa kufariki siku chache baada ya kuzaliwa wameishi karibu miaka minne na sasa wameanza kusoma katika katika shule ya Cardiff.

Marieme na Ndeye Ndiaye walipelekwa nchini Uingereza kwa matibabu kutoka Senegal mwaka 2017 na baba yao Ibrahima katika hospitali ya Great Ormond Street mjini London.

Watoto hao wa kike sasa wana miaka minne na wanajifunza kusimama, baba yao anasema kuwa wanaendelea vyema “wamepiga hatua kubwa maishani”.

Mwalimu wao mkuu amesema wamepata marafiki na “wanafuhia sana”.

Wasichana hao ambao kila mmoja ana moyo na uti wake wa mgongo lakini wanatumia ini, kibofu cha mojo na mfumo wa kusaga chakula, wanakabiliwa na hali ambayo inawaweka katika hatari inayotokana athari za ugonjwa Covid.

Hata hivyo, Bw. Ndiaye anasema alitaka waanze shule ili waendelee mbele na maisha ya kawaida.

“Unapoangalia kwenye kioo cha kutazama nyuma, Hii ni ndoto ambayo haikutarajiwa kutimia,” alisema.

“Kuanzia sasa, kila hatua tunayopiga itakuwa ni mafanikio kwangu, Moyo wangu umeridhika, ‘Tuendeleeni mbele! Tusonge mbele wanagu! Endeleeni kunishangaza!’.”

Bw. Ndiaye aliwapeleka watoto hao Uingereza kupitia ufadhili wa wakfu unaoendeshwa na Mama wa taifa la Senegal Marieme Faye Sall, kabla aombe kupewa hifadhi.

Mwezi Machi 2018, familia hiyo ilihamishwa Cardiff na ofisi ya masuala ya ndani kama waomba hifadhi ambao wanaweza kupelekwa popote nchini Uingereza tna sasa wana kibali cha hairi ya kabuki.

Mwaka 2019, Wapasuaji kutoka Great Ormond Street walitafakari uwezekano wa kuwatenganisha mapacha hao lakini Bw. Ndiaye hakuridhia hata hiyo kutokana na hatari inayohusishwa na upasuaji huo.

The twins at Ty Hafan hospice

Kutoka wakati huo madaktari wamebaini kuwa viungo vya watoto hao vimeunganika zaidi ya vile ilivyodhaniwa awali na hakuna yule anayeweza kuishi bila mwenzake, hali inayofanya kuwa vigumu kuwatenganisha.

Mwalimu mkuu wa watoto hao Helen Borley amesema wanaendelea vyema na masomo yao tangu walipojiunga na shule mwezi Septemba na wamepata marafiki.

‘Tabia tofauti’

Amesema: “Watoto hao wanasema, ‘Mimi ni rafiki wa Marieme’ au ‘Mimi ni rafiki wa Ndeye’ – Hawasemi, ‘ Mimi ni rafiki wa mapacha’. Watoto wanawatofautisha kila mmoja wao – kwa sababu wanatofautiana kwa tabia.

“Wanacheka sana – hali ambayo ni ishara nzuri,si ndio? Mtoto yeyote anayependa kucheka sana ni mtoto mwenye furaha.

The twins
Maelezo ya picha,

Marieme huwa anawekewa oksijeni kutoka kwa moyo wa Ndeye ambao una nguvu zaidi

Shule wanayosomea mapacha hao inahitaji kuendana na nyakati wanazotakiwa kwenda hospitali.

Mwezi Oktoba mwaka uliyopita, watoto hao walihitaji kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Great Ormond Street.

Dkt Gillian Body, mtaalamu bingwa wa watoto katika hospitali ya watoto ya Wales mjini Cardiff, alisema upasuaji huo ulikuwa muhimu licha ya kuwa hatari.

Alisema: “Wasichana hawa wana maumbile ya kutatanisha hali ambayo inawaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa.

“Moja ya changamoto kuu ilikuwa kupata dawa aina ya antibiotiki ambayo wanaweza kupewa kwa njia ya haraka, na suala la ni mfumo gani utatumiwa kwanza kuzingatia aina ya mpira waliyowekewa bila kuwapitishia kwenye adha ya upasuaji wa mara kwa mara ambao huenda ukawaumiza.”

Twins learning to stand

Alisema moyo wa Marieme unakabiliwa na changamoto kadhaa ambazo humfanya asiweze kufanya mazoezi hali ambayo huenda ikamfanya ashindwe kupumua.

‘Kupata usawa huo’

Walitengezewa kifaa maalum kinachowawezesha kukaa wima, kuwasidia kujenga misuli ya miguu.

Mtaalamu wa mifupa Sara Wade-West amesema ilikuwa hali ngumu kwao.

“Ni hali tofauti sana wakati umezoea kuketishwa, alafu unatakiwa kukaa wima hali ambayo huenda ni ya kuogofya ,”

“Kwanza, Ndeye hakutaka kufanya hivyo. Tulijaribu kufanya tiba hiyo wakati wa mchezo, na kujaribu kuwashawishi wachukue kitu kilicho mbali nao ili wapite kufanya mazoezi ya kuimarisha viungo vyao, lakini wakijua ni sehemu ya tiba mchezo haupendezi.

“Kutokana na utendakazi wa nyoyo zao hatuwezi kuwasukuma sana kupata uimara – tunataka wawe na nguvu lakini sio kuwachosha.”

Ibrahima Ndiaye
Maelezo ya picha,

Baba wa mapacha Ibrahima Ndiaye anasema watoto wake ni mashujaa

Kuwaona mabinti zake wakisimama ni hatua kubwa sana na ya kutia moyo kwa baba yao.

“Wanaonesha kuwa hawataki kuishi tu, lakini pia wanataka kuwa sehemu ya jamii kwa kuishi maisha ya kawaida ya kucheza na kufurahia maisha licha ya maumbile yao ,”alisema.

“Haya yote ni mafanikio ambayo yanaashiria matumaini ya siku zijazo. Lakini nafahamu kuwa ni hali tete na ambayo haiwezi kutabirika katika maisha yao.”

Bw. Ndiaye anasema matumaini yake ”yalienda sambamba na hofu yangu” wakati mwingine hali ya watoto inakaribia kuwa mbaya sana.

“Lakini kile ambacho naweza kuwafanyia ni kutafuta njia ya kuwapa matumaini,” alisema.

“Kile ambacho naweza kufanya ni kuwa karibu nao na kuishi kwa matumaini na kutokubali chochote kuzima mwanga huo wa matumaini.

“Ni mashujaa wangu. Wamethibitisha kuwa hawatakata tamaa bila kupambana. Bado tunasonga mbeIe.”

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *