img

Madiwani wajadili upungufu wa madarasa

January 5, 2021

Na Timothy Itembe MARA.

BARAZA la Madiwani wa halmashauri ya Tarime  DC mkoani Mara wamejadili ukamilishaji wa upungufu wa vyumba vya madarasa uliopo  kwa shule za sekondari na msingi.

Ikiwasilishwa ripori ya mkurugenzi,Apoll Tindwa wa halmashauri hiyo mbele ya Baraza ilisema kuwa kuna upungufu wa vyumba vya madarasa kumi na sita ili kukamilisha malengo.

Taarifa hiyo ilisema kuwa  wanafunzi 6265 wakiwemo wasichana 4098 na wavulana 3227 sawa na asilimia 79.4 walifanya mtihani wa kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2020/2021.

Mkurugenzi huyo aliomba kupatiwa fedha kutoka mfuko wa jamii (CSR) shilingi 656,160,000 kwa lengo la ukamilishaji wa miundombinu na samani za shule ili ifikapo Januari,11,2021 watoto wakaanze  masomo.

Hata hivyo kwa upande wahalmashauri ya Tarime Mjini kupitia diwani wake,Chacha Marwa Machugu alimaarufu (MUSUKUMA) ametumia nafasi hiyo kumpongeza mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime hiyo,Elias Ntiruhungwa kuwaunga mkono na kutoa mabati 432.   

Musukuma aliongeza kusema kuwa mabati hayo yanaenda kukamilisha vyumba saba vya madarasa pamoja na Nyumba moja ya utawala kwa lengo la Wanafunzi kuanza masomo  ifikapo Januari,11,2021.

“Mimi nampongeza mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime mjini,Elias Ntiruhungwa kutosapoti mabati ya ukamilishaji wa madarasa na pia shukurani hizo ziende sabamba na kwa Rais John Pombe Magufuli kuhimiza watendaji kusimamia madarasa na shukurani hizo ziwaendee wadau wote wa maendeleo waliotuungamkono pamoja na wazazi wa watoto waliochangia shuguli mbalimbali ikwemo kutoa fedha zamfukoni,wananchi kwa ujumla ambaowalituunga  mkono na kuumwa na uchungu wa elimu”alisema Musukuma.

Naye mkuu wa wilaya Tarime,Mtemi Msafiri aliwataka madiwani pamoja na watumishi kwa ujumla kutoa ushirikiano wa dhati ili kuhakikisha wanafunzi wanaenda kuanza masomo ifikapo januari,11,2021.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *