img

Kipi kitakachotokea usipooga kwa miaka mitano?

January 5, 2021

Dakika 12 zilizopita

James Hamblin

Maelezo ya picha,

Bwana Hamblin aliandika uzoefu wake wa kutooga katika kitabu alichokichapisha hivi majuzi

“Najihisi nimzima na buheri wa afya.”

Daktari James Hamblin anajibu maswali kuhusu uamuzi wake wa kutooga kwa miaka mitano.

“Unazoea. Na utakuwa unahisi kawaida kabisa,” ameiambia BBC.

Hamblin, 37, ni profesa wa chuo kikuu cha Yale shule ya Afya ya Umma na daktari ambaye amebobea katika tiba ya magonjwa yenye kinga.

Pia ni mwandishi wa jarida la Marekani la ‘The Atlantic’, ambapo alichapisha makala mwaka 2016, yakiwa na kichwa cha: “Niliacha kuoga, na maisha yakaendelea”.

“Tunatumia muda wa miaka miwili ya maisha yetu kuoga. Ushawahi kujiuliza muda huo wote ni pesa ngapi au maji lita ngapi uliopoteza?” aliandika.

Mwaka 2020, Hamblin alitoa maelezo kwa kina katika kitabu kilichopewa jina la ‘Usafi’: The New Science of Skin and the Beauty of Doing Less.

mwanamke akioga

Maelezo ya picha,

je kun aumuhimu gani wa kuoga kila siku

Kutooga kulianza kama jaribio

Uamuzi wa kutooga ulianza kama jaribio tu.

“Nilitaka kujua nini kitatokea,” anaelezea.

“Najua watu wengi ambao huoga siku moja moja. Nilijua kuwa inawezekana lakini nilitaka kujaribu mimi mwenyewe nione kitakachotokea.”

Sasa je, kuacha kuoga mwaka 2015 kulikuwa na athari gani?

“Mwili unaendelea kuzoea kadiri siku zinavyokwenda, na hivyobasi hutanuka sana ikiwa hautumii marashi wala sabuni,” anasema.

“Na pia mwili wako hautanata.”

“Watu wengi wanatumia shampoo kuondoa mafuta kwenye nywele. Ikiwa utaacha kutumia vitu hivyo, nywele zake zitaanza kuwa na ule muonekano wake wa awali kabla ya kuanza kutumia bidhaa hizo,” anaongeza.

Hata hivyo, daktari huyo anaeleza kuwa huo ni mchakato unaofanyika taratibu.

Alianza kwa kutumia shampoo, marashi na sabuni kila baada ya siku tatu kabla ya kuacha kabisa.

“Kulikuwa na wakati nilitaka kuoga kwasababu nimetamani. Nilikuwa ninanuka vibaya na kuhisi mwili wangu una nata,” Hamblin anasema.

Mwanamke akioga

Maelezo ya picha,

Hata hivyo, daktari huyo anaeleza kuwa huo ni mchakato unaofanyanyika taratibu.

“Lakini hamu hiyo pia ikaanza kupungua.”

Fikra za Hamblin ni kwamba anapoendelea kuacha matumizi ya vitu hivyo taratibu pia naye anagundua kuwa “uhitaji wake sio wa muhimu”.

Harufu ya mwili na bakteria

Daktari huyo wa Marekani anaeleza kuwa miili yetu ni chakula cha bakteria inayoishi kwenye ngozi yetu na kitamu zaidi ni jasho na mafuta tunayojipaka mwilini.

Kwa kupaka mafuta kwenye ngozi na kwenye nywele kila siku, Hambling anasema, uwiano kati ya mafuta kwenye ngozi na bakteria hutatizika.

“Unapooga kila siku, unaharibu mfumo wako wa ikolojia,” aliandika kwenye makala ya The Atlantic mwaka 2016.

“Viini huzaana kwa haraka lakini pia hali hii huonekana kujitokeza zaidi kulingana na aina ya viini vinavyoingia mwilini ambavyo hutoa harufu.”

Hata hivyo, daktari huyo amesema kuwa kutooga kunasababisha mchakato wa kila siku ambapo mfumo wa ikolojia unafika mahali na kuanza kujidhibiti wenyewe na kuacha kutoa harufu mbaya.

“Hunukii kama maji na marashi ya mwili, lakini hautatoa harufu mbaya.”

“Utanuka tu kama mtu wa kawaida,” Hamblin anasema.

Bidhaa za kuosha mwili

Maelezo ya picha,

Je mwili wa mtu unaweza kunuka asipooga?

Je mwili wa mtu unaweza kunuka asipooga?

Katika mahojiano na kitengo cha BBC Science Focus magazine Agosti 2020, Hamblin aliulizwa haoni ikiwa pengine anatoa harufu mbaya mwilini lakini watu tu ndio ambao wameamua kutomwambia lolote.

Daktari huyo alisema, amewaomba wafanyakazi wenzake, rafiki na wanaomfahamu kutosita kumwambia ukweli pale atakapoanza kunuka.

Na isitoshe, Hamblin alisema harufu yake mpya imependwa na mke wake na wengine pia hawajaichukulia kuwa mbaya.

Lakini je ni kweli Hamblin ameacha kuoga kabisa?

Anasema huwa anajimwagilia maji tu juujuu kwa uchafu ambao amepata na unaonekana kabisa au baada ya kufanya mazoezi.

Lakini pia msomi huyo anadai kuwa unaweza kuondoa ule uchafu ambao unaonekana kunata kwa kusugua kwa kutumia mikono yetu na kuchana nywele mara kwa mara.

Mwanamke mawenye ngozi ilio na madoa

Maelezo ya picha,

Mtaalamu huyo anasema kwamba utumizi wa bidhaa za kusafisha mwili husababisha ukosefu wa usawa wa viini vinavyoishi katika ngozi zetu

Sayansi na biashara

Hamblin anadai kuwa kuna umuhimu wa kutofautisha kati ya sayansi na biashara kwasababu siku hizi kunatengenezwa bidhaa nyingi tu zaidi ya tunazohitaji kwasababu ya imani kwamba zitachangia kuwa na afya bora.

“Watu wengi hawakuwa na uwezo wa kupata maji hadi miaka 100 iliyopita,” Hamblin anasema.

“Ni kitu ambacho pengine wakati huo, ni familia za kifalme pekee zilizokuwa na uwezo wa kupata maji majumbani.”

“Pengine walienda mtoni au kwenye ziwa kila walipotaka kuoga lakini sio jambo ambalo lilikuwa lazima kutekelezwa kila siku,” ameongeza.

“Pia hakukuwa na uwezo wa kutengeneza kiwango kikubwa cha bidhaa kama sabuni kwahiyo watu wengi walijitengenezea sabuni majumbani na hazikutumiwa kila siku kwasababu zilikuwa zinawasha mwili.”

James Hamblin

Maelezo ya picha,

Hamblin anasema hujimwagia maji kila mara anapofanya mazoezi ya kukimbia

Lakini kuoga kunafanywa kuwa muhimu kupita kiasi?

Zaidi ya yote, msomi huyo anasema fikra juu ya kuoga au nini maana ya usafi kunatofautiana baina ya watu.

Anaamini kuwa tabia ya kuoga imefanywa kuwa muhimu kupita maelezo.

“Mimi naweza kusema ni chaguo la mtu, wala sio hitaji la lazima eti kitiba.”

“(Lakini) isichukuliwe kuwa ninashauri watu wasioge,” Hamblin amesema.

sabuni

Maelezo ya picha,

Kitabu cha Hamblin ni muhimu katika soko la bidhaa za kusafisha ngozi

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *