img

Kampuni ya Total yawaondoa wafanyakazi wake ikihofia mashambulio Msumbiji

January 5, 2021

Kampuni ya mafuta ya Total imewaondoa maelfu ya wafanyakazi wakekatika visima vya mafuta vilivyopo kaskazini mwa Msumbiji baada ya wanamgambo walio watiifu kwa kundi la Islamic State kutishia kushambulia mji muhimu katika eneo hilo.

Vyombo vya habari vinasema kwamba Wanamgambo hao walisambaza vijikaratasi vinavyotishia kushambulia eneo la Palma katika mkoa wenye utajiri wa mafuta wa Cabo Delgado.

Tishio hilo lilisababisha Total kuwaondoa wafanyakazi wake katika eneo la Afunsi karibu na Palma ambapo linaongoza ujenzi wa kiwanda cha gesi chenye thamani ya $14.9bn.

Mtandao wa Carta de Mocambique umesema kwamba wapiganaji hao walikabiliana na vikosi vya serikalikaribu na palma tarehe mosi Januari.

Mkoa wa Cabo Delgado , ambapo ni nyumbani kwa rais Fillipe Nyusi , unapakana na Tanzania na umekumbwa na ghasia mbaya zilizotekelezwa na wapiganaji hao tangu 2017.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *