img

Jinsi mhamasishaji mtandaoni alivyomfanya binti yake wa miaka tisa aliyekuwa anahisi njaa, kufungua mkebe wa maharage kwa saa sita

January 5, 2021

Dakika 3 zilizopita

Bowl of beans

Baba mmoja nchini Marekani alijigamba kwenye mitandao ya kijamii kuwa alimwambia binti yake mwenye miaka tisa kufungua kopo la maharage au kutokula.

Baada ya saa sita mtoto huyo alifanikiwa kufungua mkebe na hatimaye kuruhusiwa kula, alisema katika ujumbe ambao sasa umefutwa.

Baba huyo, alidai hatua yake ilikuwa ya ushindi kwa ”ulezi bora”.

Lakini wazazi wengine walimkosoa kwa kupuuza majukumu yake, huku wengine wakisema alichukua hatua hiyo kujipatia umaarufu.

Watumiaji wa Twitter walimbatiza jina la “bean dad” baada ya kisa hicho kuzua gumzo katika mitandao ya kijamii, ambapo suala la ulezi husababisha mjadala mara kwa mara.

John Roderick, ambaye pia ni mwanamuziki, alisimulia kisa hicho kwenye Twitter siku ya Jumamosi, akielezea kuwa ilianza wakati binti yake alipomuomba amfungulie kopo la maharage.

Alipomletea kopo hilo la maharage afungue alimuuiliza ikiwa anajua jinsi kifaa cha kukata kopo kinavyotumika.

Aliposema hajua, akaamua kutumia wakati huo “kumuonesha kwa kumuangushia kifaa hicho mapajani”.

”Nilikuwa baba mwenye furaha” aliongeza kusema.

Baba huyo alielezea kwamba alitaka binti yake ajifunze jinsi ya kufungua mkebe wa maharage, alijaribu kuufungua mkebe huo kwa saa sita.

“Alikuwa karibu na mimi muda wote huo aking’ang’ana kufungua. Nataka niseme haya ni mambo ambayo hakuwa na ufahamu nayo na wale hakufikiria ningelimwambia afanye mwenyewe, Nilijua itakuwa changamoto,” alisema.

Hatimaye alifanikiwa kuufungua mkebe na kula maharage, aliendelea kusema.

Ujumbe huo ulisambazwa mitandaoni kwa kasi huku baadhi ya watumiaji wa mitandao hiyo wakilaani vikali tukio hilo, wakisema ni ulezi mbaya.

“Nadhani ni wazo la busara kuwafunza watoto kwamba hawako peke yao duniani na kwamba sio aibu kuomba watu msaada,” aliandika mwanahabari Jason Schreier.

Mtumiaji mwingine alisema mbinu ya Bw. Roderick ilikuwa ya “kijinga” – na kuongeza angelimsaidia binti yake ale kwanza Kisha amfundishe baadaye jinsi ya kufungua kopo hilo.

Lakini watu wachache waliunga mkono hatua ya Bw. Roderick wakidai alimfundisha vyema mwanawe.

“Hii inafundisha uhuru na ukuaji wa kibinafsi. Hakufanya chochote kibaya na kwa kweli alinifanya nitamani ningefanya zaidi ya hii, ” mmoja aliandika, wakati mashabiki wengine wa podcast yake walipendekeza kwamba hadithi juu ya binti yake iliandikwa kwa sauti ya mhusika kwenye onyesho lake, kwa hivyo haipaswi kuchukuliwa kwa uzito.

Bw. Roderick hakujibu ombi la vyombo vya habari la kumtaka atoe tamko kuhusiana na suala hilo lakini alijitetea kwenye Twitter kabla ya kufunga akaunti yake.

“Saa Sita ni muda kati ya saa za chakula. Chakula cha mchana saa sita, chakula cha jioni saa kumi na mbili. Wanasema ni unyanyasaji wa mtoto,”aliandika na kuongeza ukosoaji dhidi yake “unashangaza. Mwanangu hana neno.”

Lakini mwanamke aliyejitambulisha kama mwalimu alisema hiyo ni njia mbaya ya kumfundisha mtoto.

“Watoto hujifunza wakati hawana njaa. Kila mtu hufundisha kwa njia tofauti (kwa mfano. kuelekeza) ikiwa anayepewa mafunzo anahitaji msaada,” alisema.

Na mwandishi wa Racheline Maltese alisema somo alilijifunza mtoto huyo halikuwa zuri.

Baadhi ya watu pia walimlaumu Bw. Roderick kwa ubaguzi wa rangi, kijinsia na kingono baada ya kufuatilia baadhi ya mada alizoweka mitandaoni kabla ya kisa hiki.

Hata hivyo, msimulizi mwenza wa podcast Ken Jennings alimtetea Bw. Roderick, na kumsifia kuwa ” baba anayempenda mwanawe kwa dhati”.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *