img

Buhari aitisha viongozi wa Afrika Mashariki kuungana dhidi ya ugaidi

January 5, 2021

Rais wa Nigeria Mohammed Buhari amewaita viongozi wa Afrika Magharibi waungane katika vita dhidi ya ugaidi.

Msemaji wa Buhari Garba Shehu alitoa taarifa kwa maandishi baada ya mauaji ya karibu watu 100 katika shambulizi dhidi ya raia katika vijiji vya mpaka wa Mali nchini Niger.

Shehu akilaani shambulizi hilo, amesema,

“Rais wa Nigeria Mohammed Buhari ametoa wito kwa viongozi wa nchi za Afrika Magharibi kuungana katika mapambano dhidi ya ugaidi.” 

Shehu alisma kuwa mauaji ya watu wasio na hatia yalimwathiri sana, na kuongeza kwa kusema,

“Eneo la Sahel linakabiliwa na shida kubwa ya usalama kutokana na magaidi. Ugaidi unaweza kuenea kama uovu unavyoenea ikiwa hatutachukua hatua. Ni umoja tu dhidi ya maadui ambao unaweza kutusaidia.” 

Akikumbushia kwamba kupinduliwa kwa Muammar Gaddafi nchini Libya kulisababisha matatizo ya usalama katika nchi kama vile Nigeria, Niger, Chad, Cameroon na Mali, Shehu alibainisha kuwa baada ya kupinduliwa kwa kiongozi huyo, silaha nyingi zilienda katika mikono ya uhalifu.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *