img

Brad Raffensperger: Afisa mkuu wa Uchaguzi Georgia asema madai Trump hakushinda katika jimbo hilo

January 5, 2021

Dakika 4 zilizopita

Brad Raffensperger: Afisa mkuu wa Uchaguzi Georgia asema madai Trump hakushinda katika jimbo hilo
Maelezo ya picha,

Afisa mkuu wa Uchaguzi Georgia Brad Raffensperger asema madai Trump hakushinda katika jimbo hilo

Afisa wa juu Georgia Brad Raffensperger ametaja madai ya uwongo ya Donald Trump kuwa alipata ushindi wa jimbo hilo katika uchaguzi uliofanywa 2020 “makosa yalio wazi”.

Matamshi ya Bwana Raffensperger yanawadia baada ya Bwana Trump kumshinikiza katika mazungumzo ya simu yaliovuja kwamba “atafute” kura za kumuwezesha kupata ushindi.

Trump amekosolewa pakubwa huku baadhi wakidai alichofanya ni sawa na kuingilia mchakato wa upigaji kura kinyume na sheria.

Wabunge wa Republican wanahofia kuwa hatua hiyo huenda ikadidimiza juhudi zao za kupata ushindi katika uchaguzi wa maseneta wa jimbo la Georgia Jumanne.

Ikiwa Republicans watapata ushindi katika uchaguzi wa kumchagua Seneti huko Georgia kwenye marudio ya uchaguzi, wataendeleza kudhibiti bunge la juu.

Na ikiwa mgombea wao atashindwa, Democrats watachukua udhibiti wa bunge la Seneti pamoja na bunge la wawakilishi.

“Alizungumza sana. Na muda mwingi na sisi tukawa tunamsikiliza,” Bwana Raffensperger amezungumza na shirika la habari la ABC News Jumatatu.

“Lakini nilichotaka kieleweke ni kuwa takwimu alizonazo ni za uwongo.”

Alizungumza kwa simu kwa takriban saa nzima na rais akiwa na timu yake Jumamosi, na mazungumzo hayo yaliovuja yalitolewa na gazeti la Washington Post siku iliyofuata.

Jumatatu, Bwana Raffensperger aliwaambia wanahabari kwamba hakujua kuwa mazungumzo yao yanarekodiwa na alizungumza na rais akiwa nyumbani kwake.

Donald Trump

media captionDonald Trump: “I just want to find 11,780 votes”

“Bwana Trump alikuwa na mamia na mamia ya watu waliompigia kura ambao walishafariki dunia. Tulipata majina ya watu wawili, huo ni mfano tu kwamba takwimu alizonazo sio sahihi,” aliongeza.

Gabriel Sterling, mkuu anayesimamia mfumo wa upigaji kura jimboni humo, alisema Jumatatu katika mkutano wa wanahabari kuwa madai ya Bwana Trump ni ya “uwongo mtupu”.

Pia alisikitishwa na simu hiyo ya aliyompigia Bwana Raffensperger.

Bwana Sterling alionya kuwa rais anashukisha kiwango cha uaminifu kwa raia wa Georgia katika mchakato wa uchaguzi na kusihi wakazi wajitokeze kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi wa Jumanne.

“Kura ya kila mmoja wenu itahesabiwa,” amesema.

Alisema nini kwenye simu iliyovuja?

Bwana Trump anasikika akimshinikiza katibu wa jimbo la Georgia kuhesabu tena kura.

“Nataka tu kupata kura 11,780,” amesema. Idadi hiyo ingemwezesha kupata kura 2,473,634 katika jimbo hilo, ikiwa ni moja tu zaidi ya mpinzani wake wa chama cha Democratic Rais mteule Joe Biden, aliyepata kura 2,473,633.

Pia amemshutumu Bwana Raffensperger – ambaye ni wa chama cha Republican – kwa kuharibu kura na kujihusisha na vitendo vya uhalifu ambavyo vilichangia Trump kushindwa kwenye uchaguzi wa jimbo hilo. Ametaja madai hayo ya uwongo “kosa la uhalifu,” na kuongeza kuwa ni hatari kubwa kwake.

Bwana Raffensperger alijibu kwa kusema kuwa kampeni ya Trump imeshindwa katika kesi nyingi ilizowasilisha mahakamani.

“Changamoto yako Bwana Rais, ni kwamba data ulionayo sio sahihi.”

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *