img

Boris Johnson atangaza vikwazo vipya kupambana na COVID-19

January 5, 2021

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametangaza vikwazo vipya vya kuzuia kasi ya maambukizi ya virusi vya corona nchini England, ambavyo vinaweza kubakia hadi katikati mwa mwezi Februari. 

Johnson amesema nchi hiyo inapita katika kipindi kigumu, ambapo maambukizi ya aina mpya ya virusi yanasambaa kwa kasi katika maeneo yote. 

Kulingana na vikwazo hivyo vipya, shule za msingi na sekondari zitafungwa, na vyuo vikuu havitafunguliwa hadi angalau katikati ya Februari.

 Maduka ya bidhaa na huduma zisizo za lazima pia yataendelea kufungwa. Hadi jana Jumatatu England ilikuwa na wagonjwa 26,626 wa COVID-19 waliolazwa hospitalini, hilo likiwa ongezeko la asilimia 30 ikilinganishwa na wiki iliyopita. 

Akilihutubia taifa jana jioni, Boris Johnson alisema anatumai vikwazo hivyo ni hatua za mwisho katika kupambana na janga la virusi vya corona.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *