img

Assange yuko huru kurejea nyumbani, asema Waziri Mkuu wa Australia

January 5, 2021

Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison amesema leo kuwa Julian Assange yuko huru kurejea nyumbani baada ya kutatua matatizo yake ya kisheria. Morrison ameyasema hayo baada ya mahakama ya Uingereza jana kupinga ombi la kutaka muasisi huyo wa shirika la kimataifa la ufichuzi WikiLeaks ahamishiwe Marekani. 

Waziri Mkuu wa Australia amesema mfumo wa sheria unafanya kazi yake na kuwa nchi haiwezi kuingilia kwa sasa. Lakini Assange, kama raia mwingine yeyote wa Australia, ana haki ya kupewa msaada ubalozini na kuwa baada ya kesi yake, yuko huru kurejea nyumbani. 

Assange, mwenye umri wa miaka 49, ameshitakiwa Marekani kwa makosa 18 wakati wa utawala wa Rais wa zamani Barack Obama yanayohusiana na uvujishaji uliofanywa na tovuti ya WikiLeaks wa nyaraka za siri za jeshi la Marekani na za kidiplomasia ambazo wanasema ziliyaweka maisha ya watu hatarini.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *