img

Alibaba: Jinsi tajiri wa China Jack Ma alivyopoteza dola bilioni 11 ndani ya miezi miwili

January 5, 2021

Dakika 10 zilizopita

Masaibu ya Jack Ma yalianza pale ambapo mojawapo ya mikataba yake ilishindwa kufanikiwa

Maelezo ya picha,

Masaibu ya Jack Ma yalianza pale ambapo mojawapo ya mikataba yake ilishindwa kufanikiwa

Tajiri wa China Jack Ma amefunga mwaka vibaya.

Tajiri huyo mwanzilishi wa kampuni ya Alibaba, moja kati ya wafanyabiashara tajiri barani Asia amepoteza karibu dola bilioni 11 tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba, pale mamlaka ilipoanza kuuchunguza kampuni yake pamoja na makampuni mengine makubwa ya teknolojia.

Mwaka huu utajiri wa Ma ulifika bilioni 61.7 na alikuwa karibu kwa mara nyingine tena kuwa mtu tajiri zaidi nchini China.

Hata hivyo, utajiri wake ulipungua kwa bilioni 50.9, kulingana na kipimo cha mabilionea cha Bloomberg ambacho kilimuweka katika nafasi ya nne.

Matatizo ya mfanyabiashara huyo yalianza pale moja ya kampuni zake kubwa: Grupo Hormiga IPO ilipoanza kuandamwa na serikali.

Mwanzoni mwa Novemba, kila kitu kilikuwa sawa kwa kile ambacho kingekuwa makubaliano makubwa ambayo yangeweka historia kilibadilika na kwenda segemnege.

Na baadhi ya shughuli za kampuni hiyo zikakatizwa ghafla dakika za mwisho na mamlaka ya udhibiti wa shughuli za fedha.

Baadhi ya wachambuzi walifasiri hilo kama hatua ya China kudhibiti ukuaji wa kampuni kubwa kama yake hasa kutokana na tabia ya kampuni anazomiliki na hata Ma mwenyewe ya kutoa matamshi yanayoonekana kukosoa serikali, kulingana na mwandishi habari wa BBC, Tomothy McDonald kutoka Singapore.

“Ma alianza kutoka akiwa nembo ya China kama yenye uwezo na maendeleo ya kiteknolojia hadi kuwa tishio.”

Tajiri huyo huenda alikasirisha mamlaka ya China pale alipokosoa hadharani benki za China zinazomilikiwa na serikali na kuzilinganisha na “maduka ya kuweka kitu rehani” yasio na ubunifu wowote.

Nguvu ya shughuli za fedha mtandaoni

Na kuanzia hapo, mambo yakaanza kuwa magumu kwa kampuni ya Grupo Hormiga, muungano wa makampuni anaomiliki ambao umekua kwa haraka miaka ya hivi karibuni.

Huduma maarufu sana iliyoanzisha ni ile ya Alipay, kama jukwaa la malipo kwa huduma zinazotolewa na kampuni ya Alibaba.

Ma aliikosoa hadharani serikali ya China

Kampuni hiyo inachukua pesa za wanunuaji kwa uaminifu kuwa watapokea bidhaa zao walizonunua kwa njia ya mtandao.

Huduma ya Alipay ilikuwa muhimu katika ukuaji wa kampuni ya Alibaba. Na sasa hivi ndio inayotumika zaidi nchini China kuliko mfumo wa kulipia huduma kwa kutumia kadi.

Kampuni ya IPO iliposimamishwa kuendeleza shughuli zake, Soko la Hisa la Hong Kong likaeleza kuwa hiyo ni kwasababu kampuni ya Grupo Hormiga “huenda haikutimiza viwango vya uwazi vinavyohitajika kuwezesha kuorodhwesha” na kusema kuwa “mabadiliko ya hivi karibuni” kwenye udhibiti wa shughuli za kifedha zinazofanywa mitandaoni ndio kikwazo.

“Yalikuwa makubaliano mazuri na makubwa. Lakini sidhani kama China itakubali makubaliano yoyote ya aina hiyo. Haiwezi kuhatarisha mfumo wake wa kifedha kwa makubaliano ya aina hiyo, ” amesema Drew Bernstein, mkurugenzi wa kampuni ya Marcum Bernstein & Pinchuk, inayotoa ushauri kwa kampuni za China.

Je kuna ushindani usio wa haki?

Siku kadhaa zilizopita Benki ya Kuu ya China iliagiza kampuni ya Jack Ma ya Grupo Hormiga kufanya mabadiliko, ili iweze “kurekebisha” mikopo yake, bima yake na huduma zake za usimamizi wa mali.

Kulingana na naibu gavana wa Benki ya China, Pan Gongsheng, wadhibiti wanachunguza “usimamizi mbaya wa kampuni ya Grupo Hormiga”, ukiukaji wa baadhi ya masharti na tabia yake ya kutaka kulazimisha kushinda washinda wake ili kuhakikisha kunakuwa na ushindani wa haki.

Huduma ya Ant ambayo ni maarufu kama Alipay ilianza kama huduma inayotumiwa na alibaba kufanya malipo

Maelezo ya picha,

Huduma ya Ant ambayo ni maarufu kama Alipay ilianza kama huduma inayotumiwa na alibaba kufanya malipo

Kampuni ya Grupo Hormiga imesema katika taarifa kwamba itaanzisha kitengo maalum kuboresha mabadiliko yaliyowekwa na kutekeleza kikamilifu mahitaji ya mamkala ya udhibiti.

Hata hivyo baadhi ya wataalamu wanaamini kuwa masharti mapya ya mamlaka ya udhibiti yanamlenga Ma, huku wengine wakiamini kuwa mabadiliko katika sekta ya fedha nchini China ni malengo la muda mrefu ya serikali na hayalengi kwa namna yoyote ile kampuni ya mtu fulani.

Ingawa kampuni ya Jack Ma ndio inayotoa huduma ya malipo ya mtandaoni kwa kiasi kikubwa mno nchini China ikiwa na watumiaji zaidi ya milioni 730 katika huduma yake ya Alipay, ndio kampuni yenye kuhusika na masuala fedha ambayo inaonekana kutiliwa mashaka zaidi ya mamlaka.

Ma sio yeye peke yake

Hata hivyo ingawa kampuni ya Jack Ma imejikuta kwenye mgogoro na mamlaka ya udhibiti wa masuala ya fedha sio ya kwanza kukumbana na hali hii.

Baadhi ya makampuni tayari yameanza kufanya mabadiliko katika utekelezaji wa shughuli zake pengine kwa kukisia kuwa huenda pia nazo zikajikuta katika mabadiliko mapya yanayohitaji.

Jack Ma

Mfano kampuni za JD Digits, Tencent, Baidu na Lufax ziliacha kuuza bidhaa zenye riba katika mitandao yao ya kibiashara baada ya mamlaka kuilazimisha kampuni ya Grupo Hormiga kufanya hivyo.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *