img

Al-Qaeda lakiri kutekeleza shambulio dhidi ya wanajeshi Mali

January 5, 2021

Tawi la kundi la kigaidi la Al-Qaeda nchini Mali, Jamaat Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM), limekiri kuhusika na mlipuko wa bomu kandokando ya barabarasiku ya Jumamosiambao uliwaua wananjeshi wawili wa Ufaransakatika eneo la mashariki la Menaka.

Madai hayo yalisambazwa na wafuasi wa kundi hilo katika mtandao wa telegram.

Wanajeshi wawili wa Ufaransawalifariki nchini Mali wakati gari lao liliposhambuliwa na kilipuzi.

Wawili hao walikuwa katika eneo la Menaka wakifanya upelelezi , ilisema afisa ya rais wa Ufaransa.

Shambulio hilo linajiri siku kadhaa tu baada ya wanajeshi wengine wa Ufaransa kufariki kwa njia kama hiyo.

Ufaransa ina takriban wanajeshi 5100 katika eneo la Sahelambalo limekuwa likiongozakatika vita hivyo dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu kwa takriban muongo mmoja sasa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *