img

Afisa mkuu wa Uchaguzi Georgia asema Trump ni muongo hakushinda katika jimbo hilo

January 5, 2021

Afisa wa juu Georgia Brad Raffensperger ametaja madai ya uwongo ya Donald Trump kuwa alipata ushindi wa jimbo hilo katika uchaguzi uliofanywa 2020 “makosa yalio wazi”.

Matamshi ya Bwana Raffensperger yanawadia baada ya Bwana Trump kumshinikiza katika mazungumzo ya simu yaliovuja kwamba “atafute” kura za kumuwezesha kupata ushindi.

Trump amekosolewa pakubwa huku baadhi wakidai alichofanya ni sawa na kuingilia mchakato wa upigaji kura kinyume na sheria.

Wabunge wa Republican wanahofia kuwa hatua hiyo huenda ikadidimiza juhudi zao za kupata ushindi katika uchaguzi wa maseneta wa jimbo la Georgia Jumanne.

Ikiwa Republicans watapata ushindi katika uchaguzi wa kumchagua Seneti huko Georgia kwenye marudio ya uchaguzi, wataendeleza kudhibiti bunge la juu.

Na ikiwa mgombea wao atashindwa, Democrats watachukua udhibiti wa bunge la Seneti pamoja na bunge la wawakilishi.

“Alizungumza sana. Na muda mwingi na sisi tukawa tunamsikiliza,” Bwana Raffensperger amezungumza na shirika la habari la ABC News Jumatatu.

“Lakini nilichotaka kieleweke ni kuwa takwimu alizonazo ni za uwongo.”

Alizungumza kwa simu kwa takriban saa nzima na rais akiwa na timu yake Jumamosi, na mazungumzo hayo yaliovuja yalitolewa na gazeti la Washington Post siku iliyofuata.

Jumatatu, Bwana Raffensperger aliwaambia wanahabari kwamba hakujua kuwa mazungumzo yao yanarekodiwa na alizungumza na rais akiwa nyumbani kwake.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *