img

Yanga kumchomoa beki wa Biashara United

January 4, 2021

 BEKI wa kutegemewa ndani ya kikosi cha Biashara United, Abdulmajid Mangalo anayekipiga ndani ya Biashara United anatajwa kuingia rada za Yanga.

Beki huyo ambaye ni nahodha pia ni mhimili ndani ya Biashara United inayonolewa na Kocha Mkuu, Francis Baraza.

Ni chaguo la kwanza la Baraza ambaye amekuwa akiweka wazi kwamba ni miongoni mwa wachezaji ambao wanatumia nguvu pale panapohitajika na akili ndani ya uwanja.

Yanga imepanga kuongeza nguvu kidogo kwenye safu ya ulinzi inayoongozwa na Lamine Moro mwenye mabao manne na pasi moja ili kuwa na uhakika wa yule anayeanza kuwa ni moto na yule atakayekuwa benchi kuwa na ubora.

Habari zinaeleza kuwa mpango mkubwa kwa sasa umeshikiliwa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze hivyo akikubali kwamba anamhitaji beki huyo basi viongozi wanamaliza kukamilisha dili ambalo walianza nalo mapema kabla ya dirisha dogo kufunguliwa.

Tayari Yanga imekamilisha usajili wa mchezaji mmoja pekee ambaye ni Saido Ntibanzokinza na kwa sasa nguvu wanazipeleka kwenye Kombe la Mapinduzi ambalo linatarajiwa kuanza leo, Januari 4.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa mipango ya usajili ipo mikononi mwa kocha.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *