img

Waliofariki kutokana na mashambulizi ya vijiji Niger wafikia 100

January 4, 2021

Waziri Mkuu wa Niger amesema watu 100 wameuawa kwenye mashambulizi ya Jumamosi yaliotekelezwa na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Wajihad katika vijiji viwili.

Brigi Rafini amesema watu 70 waliuawa katika kijiji cha Tchombangou huku wengine 30 wakiuawa katika kijiji cha Zaroumdareye – vyote vikiwa karibu na mpaka na Mali.

Hilo ni moja ya shambulizi baya zaidi kutokea wakati ambapo nchi hiyo inaendelea kupambana na vita vya kikabila na wanamgambo wa Kiislamu.

Hadi kufikia sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na mauaji hayo.

Kulingana na meya wa eneo Almou Hassane, waliohusika walisafiri kwa kutumia pikipiki 100,” kulingana na shrika la habari la AFP

Inasemekana kwamba wanamgambo hao waligawanyana katika makundi mawili na kutekeleza mashambulizi hayo kwa wakati mmoja.

Aliyekuwa waziri Issoufou Issaka ameliambia shirika la AFP kwamba wapiganaji wa jihadi walitekeleza mashambulizi hayo baada ya wanavijiji kuwaua wanachama wao wawili ingawa hiilo halijathibitishwa rasmi.

Meya Hassane amesema baada ya mashambulizi hayo wanavijiji 75 waliachwa wakiwa na majeraha huku wengine wakipelekwa kupata matibabu katika eneo la Ouallam mji mkuu wa Niamey.

Waziri Mkuu Rafini alitembelea vijiji hivyo Jumapili.

“Hali ni mbaya… lakini uchunguzi utafanywa ili waliohusika waweze kukabiliwa kisheria,” amewaambia wanahabari.

Eneo la Tillabéri huko Niger, lipo mpaka wa pande tatu Niger, Mali na Burkina Faso, ambalo kwa miaka mingi limekuwa likishambuliwa na wanamgambo wa jihadi

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *