img

Wahanga wa shambulizi la Somalia waletwa

January 4, 2021

Majeneza ya wafanyikazi wa Kituruki Selami Aydoğdu na Erdinç Genç, waliopoteza maisha katika shambulizi la kigaidi nchini Somalia, na wafanyikazi 4 ambao walijeruhiwa katika tukio hilo walirudishwa nchini kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki (THY).

Ömer Aydoğdu, mmoja wa wafanyikazi waliojeruhiwa ambaye aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Istanbul na ndege iliyounganishwa Djibouti, kutokea Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, aliwaambiawaandishi wa habari kuwa shambulizi hilo lilitokea wakati wa shughuli ya utandazaji wa lami.

Akielezea kwamba walianguka chini kutokana na mlipuko huo, Aydoğdu alisema,

“Tulikuwa tukifanya kazi kama baba na mtoto. Nimepoteza mtoto wangu katika shambulizi hilo. Ni maumivu makubwa.”

Aydoğdu pia alisema walikuwa jumla ya watu 6 waliotokea Çorum na kwenda kufanya kazi nchini Somalia.

Yavuz Ercan, ambaye pia alijeruhiwa katika shambulizi hilo, alifahamisha kuwa shambulizi lilikuwa la kusikitisha sana lakini walinusurika na kusema,

“Tumepoteza ndugu zetu, inasikitisha sana. Natamani isingefanyika, lakini hakuna la kufanya.”

Imdat Uzuncaköşe, ambaye pia alijeruhiwa katika tukio hilo alielezea masikitiko yake kwa kuzuka kwa shambulizi hilo.

Irakir Çetinkaya, ambaye alijeruhiwa mguu katika shambulizi hilo, alipelekwa hospitalini na maafisa kwa machera.

Majeneza yenye miili ya Aydoğdu na Genç yalipelekwa katika mji wao wa Çorum.

Katika shambulizi la kigaidi lililoendeshwa dhidi ya kampuni ya Uturuki nchini Somalia mnamo Januari 2, raia 2 wa Kituruki walifariki na wengine 4 walijeruhiwa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *