img

Virusi vya corona: Walimu Kenya wahofia afya yao huku shule zikifunguliwa

January 4, 2021

Dakika 12 zilizopita

Shule nchini kenya zafunguliwa

Mamilioni ya watoto nchini Kenya wanarudi katika shule za msingi na zile za upili huku kukiwa na masharti yanayolenga kupunguza maambukizi ya virusi vya corona.

Wanafunsi wa kidato cha nne wamekuwa wakiendelea na masomo yao tangu mwezi Oktoba lakini walichukua likizo fupi wakati wa likizo ya Disemba.

Baadhi ya wanafunzi katika shule za kibinafsi hatahivyo watalazimilka kusalia majumbani baada ya wamiliki wa shule hizo kuzibadilisha na kuzifanya maeneo ya biashara.

Hali hiyo inawalazimu wanafunzi waliokuwa katika shule zilizofungwa kutafuta maeneo mbadala.

Cha kusikitisha ni kwamba wazazai wengi wana wasiwasi kuhusu hali ya usalama wa wanao huku wengi wakishindwa kutafuta karo na kununua vifaa vya kusomea.

Wengine wanalalamika kwamba kufungwa kwa sehemu nyingi za kufanyia kazi mbali na masharti makali ya kukabiliana na virusi vya corona yaliotolewa na serikali kumesababisha hali ngumu ya kiuchumi.

Je walimu wanasemaje?

Tayari Mkuu wa Muungano wa walimu nchini Kenya KNUT Wilson Sossion ameonyesha kutoridhishwa kwake kuhusu usalama wa wanfunzi na walimu huku shule nchini zikifunguliwa.

Sossion amesema kwamba maandalizi yaliopo kukabiliana na virusi vya corona hayatoshi katika mahojiano yake na kipindi cha redio cha BBC NewsDay.

Bwana Sossion amesema kwamba shule za siku ambazo ni nyingi zaidi ya zile za mabweni zitaathirika kwa kuwa nyingi hazina maji na luosha mikono.

Amesema kwamba serikali haijatoa fedha kwa shule kwa ununuzi wa vifaa vya kuwapima wanafunzi , vitakasa mikono ma vifaa vingine vinavyohitajika.

”Unapotoa ujumbe kama huo kwa shule na hujazipatia ufadhili …je watatekeleza vipi masharti hayo”.?

Wanafunzi katika shule za msingi na zile za upili walirudi shuleni siku ya Jumatatu.

Wizara ya elimu imetoa wito kwa walimu kutumia kila fursa ikiwemo kusoma chini ya miti ili kuweza kufuata sheria ya kutokaribiana.

Wanafunzi wakiendelea na masomo yao darani
Wanafunzi wengine watafurahia kukutana tena na wenzao

Masharti yaliowekwa na serikali katika kila shule

  • Wazazi wametakiwa kuwanunulia watoto wao barakao huku serikali ikiahidi kusambaza baadhi ya vfaa hivyo kwa wanafunzi kutoka jamii masikini.
  • Shule zinatoa maji safi katika lango lake kuu , huku wanafunzi wakitakiwa kuosha mikono na sabuni kabla ya kuingia , kuvalia barakoa mbali na kufanyiwa vipimo vya kiwango cha joto mwilini.
  • Wanafunzi wanaopatikana na dalili zinazohusishwa na virusi vya corona wanatengwa na kupelekwa katika eneo tofauti la shule wakisubiri kurudishwa nyumbani.
  • Vilevile walimu walio na zaidi ya umri wa miaka 58 na wale walio na maradhi wametakiwa kufanya kazi kutoka nyumbani na katika maeneo yalio wazi.

Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumapili aliongeza muda wa kutotoka nje nyakati za usiku kwa miezi mingine mitatu.

Taifa limerekodi wagonjwa 98,802 wa virusi vya corona ikiwemo vifo 1,685, kulingana na wizara ya afya.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *