img

Virusi vya Corona: Ujerumani kuongeza muda wa vikwazo hadi Januari 31

January 4, 2021

 

Serikali kuu ya Ujerumani na viongozi wa majimbo 16 ya nchi hiyo wamekubaliana kuongeza muda wa hatua za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Covid-19 hadi Januari 31, gazeti la Ujerumani la Bild limeripoti.

Chini ya hatua za sasa ambazo zimekuwepo tangu Disemba 16, maduka mengi, mikahawa na baa zimefungwa.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na viongozi wakuu wa majimbo 16 wanatarajiwa kujadili hatua mpya kesho Jumanne.

Wakati huo huo, hali ya ukataji tamaa inaongezeka nchini humu kutokana na kasi na mpangilio wa utoaji chanjo ya covid-19, hatua iliyovilaazimu vyama viwili vya siasa – Chama mshirika serikalini cha SPD na kile cha FDP kutaka majibu kutoka kwa kansela Angela Merkel.

 Katibu mkuu wa chama cha SPD Lars Klingbeil, amemlaumu Waziri wa Afya Jens Sphan kwa kujikokota katika mpango wa utoaji wa chanjo. 

Spahn pia amelaumiwa na naibu kiongozi wa FDP bungeni Michael Theurer, aliemtaka aombe radhi kwa changamoto za chanjo na vurugu za serikali.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *