img

Uwanja wa Mwanakalenge Bagamoyo kuboreshwa

January 4, 2021

Na Omary Mngindo, Bagamoyo

UWANJA Mkongwe wa Mpira wa Miguu wa Mwanakalenge uliopo Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani, unataraji kuboreshwa baada ya kumalizika Ligi ngazi ya Mkoa hatua ya tisa bora chini ya Chama Cha Mpira wa Miguu mkoani hapa COREFA.

Uwanja huo wa miaka mingi unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani hapa, pamoja na kuwa katika mazingira yasiyoridhisha lakini umekuwa msaada mkubwa kwa ajili ya Ligi na mashindano mbalimbali, ambapo mashabiki lukuki wanahudhuliwa michuano hiyo.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo hilo Muharami Mkenge, akijibu maswali ya Waandishi waliotaka kufahamu mikakati iliyopo, baada ya mchezo wa Ligi tisa bora ngazi ya Mkoa, kati ya Kiembeni Fc na Dunda Fc uliomalizika kwa Dunda kushinda 2-1.

Mkenge alisema kuwa uwanja huo maarufu wilayani hapa na Mkoa kwa ujumla ambao ni mali ya chama hicho, pamoja na kutumika kwa michezo hiyo lakini una changamoto kuanzia eneo la kuchezea mpira na ukuta unaozunguka.

“Nitakaa na viongozi wenzangu wa chama kuona namna gani tutavyoweza kuanza kuuboresha, kwa kuanzia na kujaza kifusi eneo la kuchezea kisha kupanda nyasi, baada ya hatua hiyo nyingine zitafuata,” alisema Mkenge. 

Aliongeza kwamba ndani ya jimbo na wilaya nzima kwa ujumla kuna viwanja vingi lakini cha Mwanakalenge nsio tegemeo kubwa, hivyo kuna kila sababu ya kuimarishwa ili kiwe na ubora zaidi kwa ajili ya michezo mbalimbali ikiwemo Ligi za TFF.

“Pia nitumie fursa hii kuwaomba wana-Bagamoyo kutumia kipindi hiki cha Ligi hii ngazi ya Mkoa hatua ya tisa bora, wajitikeze kwa wingi kushuhudia michuano hii kwa ni hapa kuna timu kutokana wilaya na majimbo mbalimbali,” alisema Mkenge.

Mbunge huyo alizitakia heri timu zote zinazoshiriki kinyang’anyiri hicho, huku akiziombea dua zinazotokea Bagamoyo ambazo ni Baga United na Kiembeni Fc za Jimbo hilo, huku Chalinze na Msata United zinazotokea Chalinze ili zifanye vizuri zaidi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *