img

Uchaguzi wa Marekani 2020: Mazungumzo ya Trump ya siri Georgia kujaribu kubadilisha uchaguzi yanaswa

January 4, 2021

Dakika 8 zilizopita

Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump amerekodiwa akimwambia afisa mkuu wa uchaguzi Georgia atafute kura za kutosha kuwezesha kubadilishwa kwa matokeo ya uchaguzi.

“Nataka tu kupata kura 11,780,” Bwana Trump alimwambia katibu wa chama cha Republican Brad Raffensperger jimboni humo katika mazungumzo yaliyorekodiwa na kutolewa na gazeti la Washington Post.

Bwana Raffensperger anasikika akijibu kuwa matokeo ya uchaguzi ya Georgia yalikuwa sawa.

Joe Biden alishinda uchaguzi wa Georgia pamoja na majimbo mengine muhimu na kumuwezesha kupata kura 306 za wajumbe dhidi ya Bwana Trump aliyepata kura 232.

Tangu uchaguzi uliofanywa Novemba 3, Bwana Trump amekuwa akidai kuwa kura ziliibwa bila kutoa ushahidi wowote unaothibitisha madai yake.

Majimbo yote 50 yamethibitisha matokeo ya uchaguzi huo baadhi ya vituo ikiwa ni baada ya kura kuhesabiwa tena au pia kwasababu ya kesi zilizowasilishwa mahakamani kupinga matokeo.

Hadi kufikia sasa, Marekani imetupilia mbali kesi 60 zilizokuwa zimewasilishwa kupinga ushindi wa Bwana Biden.

Aidha bunge linatarajiwa kuidhinisha rasmi matokeo ya uchaguzi huo Januari 6.

Bwana Biden wa chama cha Democrat, anatarajiwa kuapishwa kama rais wa Marekani Januari 20.

Pia, wapiga kura huko Georgia wanatarajiwa kupiga tena kura Jumanne kuchagua maseneta wawili wa jimbo hilo na matokeo ya uchaguzi huo huenda yakaweka sawa jinsi nguvu ya uongozi itakavyokuwa katika bunge la Seneti.

Ikiwa washindani wawili wa chama cha Democrat watashinda, kuna maanisha kwamba kutakuwa na idadi sawa ya wabunge wa vyama vya Republican na Democratic na makamu mteule wa chama cha Democratic Kamala Harris ndiye atakayekuwa na usemi katika kura ya kufanya maamuzi.

Bwana Biden wa chama cha Democrat tayari anadhibiti bunge la wawakilishi.

Nini kilichotokea katika simu ya Trump?

Katika kipande kilichotolewa na gazeti la Washington Post, Bwana Trump anasikika akisema pengine njia nyingine ni kumshawishi na kumshinikiza katibu wa jimbo la Georgia.

Alisisitiza kuwa ameshinda uchaguzi katika jimbo la Georgia na kumuambia Bwana Raffensperger kwamba hakukuwa na ubaya wowote kusema kuwa “mumehesabu kura tena”.

Bwana Raffensperger alijibu kwa kusema: “Changamoto uliyonayo Mheshimiwa Rais ni kwamba takwimu ulizonazo wewe ni za uwongo.”

Baadaye katika simu hiyo, Bwana Trump alisema uvumi uliopo ni kuwa kura zilizopigwa kwa njia ya posta zimeharibiwa na mashine ya kupiga kura iliondolewa kutoka kaunti ya Fulton jimboni humo – dai ambalo wakili wa Bwana Raffensperger amesema sio sahihi.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *