img

Tetesi za soka kimataifa

January 4, 2021

 

Kazi ya ukufunzi ya Frank Lampard kama meneja awa Chelsea inakabiliwa na changamoto kubwa na sasa klabu hiyo imeanza kutafuta njia. (The Athletic – subscription required)

Tottenham wameanzisha mazungumzo ya mapema na mshambuliaji Harry Kane kuhusu kuongezwa kwa kandarasi yake. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 na nahodha wa England alitia saini kandarasi ya miaka sita mwaka 2018 lakini mwenyekiti Daniel Levy anataka kufunga hamu inayowasilishwa na Manchester City pamoja na Paris St-Germain. (Independent)

Paris St-Germain imeanza mazungumzo na Everton kubadilisha kandarasi ya mkopo ya mshambuliaji wa Itali Moise Kean kwa mkataba wa kudumu wenye thamani ya £31m. (Sky Sports)

Mkufunzi mpya wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino ataruhusiwa kukifanyia mabadiliko kikosi chake na hiyo inamaanisha kwamba huenda akamsajili kiungo wa kati wa Tottenham na England Dele Alli. (Mirror)

Mkufunzi wa Paris St-Germain Pochettino ameawasiliana na Dele Alli, ambaye alikuwa mchezaji maarufu chini ya usimamizi wake katika klabu ya Tottenham. (Foot Mercato – in French)

Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 27, ambaye alikuwa amehusishwa na uhamisho wa Tottenham na Manchester United, atauzwa na Juventus mwisho wa msimu huu iwapo atakataa kutia saini kandarasi. (Tuttosport via Football Italia)

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer atafanya mazungumzo na wachezaji kadhaa katika mipango yake ya dirisha la uhamisho la mwezi Januari na wachezaji sita huenda wakaondoka kwa mkopo ama kwa kandarasi za kudumu. (Sun)

Manchester United itakataa jaribio la klabu ya Atalanta kumzuia winga wa Ivory Coast Amad Diallo, 18, katika klabu hiyo ya Serie A hadi mwisho wa msimu huu . (ESPN)

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anasema kwamba klabu hiyo itazungumzia hatma ya mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 Alexandre Lacazette mwisho wa msimu huu. (Standard)

Beki wa Ufaransa Lucas Digne, 27, anakaribia kuandikisha mkataba mpya na Everton. (Liverpool Echo)

Arsenal iko tayari kumrudisha nyumbani kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira kutoka uhamisho wake wa mkopo huko Atletico Madrid, huku klabu ya Fiorentina ikiimarisha hamu ya kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (La Nazione via Express)

Kiungo wa kati wa Uhispania Joan Jordan, 26, anasema kwamba anaendelea vyema katika klabu ya Sevilla, huku akihusishwa na uhamisho wa kwenda Arsenal. (Football London)

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *