img

TAKUKURU Manyara yaonya baadhi ya watu wanowalaghai Wakulima

January 4, 2021

Na John Walter-Manyara

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Manyara imeonya baadhi ya watu wanaowalaghai wakulima katika Wilaya ya Kiteto kutokurejesha mikopo ya matrekta kutoka shirika la Maendeleo ya taifa (NDC) yenye thamani ya shilingi bilioni 7.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Manyara Holle Makungu akizungumza na Muungwana Blog amesema kuwa tayari wameanzisha uchunguzi kwa wanaohusika na ulaghai huo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Aidha Takukuru imewataka wananchi pamoja na viongozi kutumia nafasi zao vizuri kuhakikisha fedha zilizotolewa na serikali zinarejeshwa na si vingnevyo.

Kwa upande wao wakazi wa Mkoa wa Manyara  Yasinta Simwita amesema kuwa ushirikiano unahitajika kuwafichua wenye nia mbaya na mikopo inayotolewa na serikali.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *